Mafanikio makubwa tunayoendelea kuyapata yanatokana na bidii pamoja na ueledi wa wafanyakazi wetu na tunafuraha kutambulika kama Mwajiri Bora nchini Tanzania katika Tuzo zilizotolewa na Chama cha Waajiri Tanzania (ATE) - 2023 jana jijini Dar es Salaam.

Tuzo hizo ni:

✅ Mwajiri Bora anaezingatia Ubora, Uzalishaji na Ubunifu Pahala pa Kazi 2023

✅ Mwajiri Bora anaezingatia Usawa wa Kijinsia na Usawa katika Uwakilishi Pahala pa Kazi 2023

✅ Mwajiri Bora wa Jumla (Mshindi wa Pili) kwa Sekta Binafsi kwa Mwaka 2023

✅ Mwajiri Bora wa Jumla (Mshindi wa pili) kwa mwaka 2023.

Tuzo hizo kwa ujumla wake zinatambua weledi wa benki yetu katika kufata misingi bora ya utumishi huku tukiwajengea wafanyakazi wetu mazingira wezeshi ya kiutendaji.

Tuzo hizi zimetolea na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) - Prof. Joyce Ndalichako aliyemuwakilisha Waziri Mkuu - Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa na zimepokelewa na Afisa Mkuu wetu wa Rasilimali Watu - Emmanuel Akonaay pamoja na Mkuu wetu wa Idara ya Rasilimali Watu - Joanitha Rwegasira Mrengo, walioambatana na wafanyakazi wengine.

Tunawashukuru wafanyakazi wetu kwa kuendelea kuwa msingi wa mafanikio yetu.


#NMBKaribuYako

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...