Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Ushirikiano wa Elimu Duniani (GPE), Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, akiwa na Afisa Mtendaji Mkuu wa GPE, Bibi Laura Frigenti, wakipata picha ya kumbukumbu na baadhi ya wafanyakazi wa hoteli ya Kilimanjaro Hyatt jijini Dar es salaam leo asubuhi.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Ushirikiano wa Elimu Duniani (GPE), Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, akisindikizwa na Waziri wa Elimu Profesa Adolf Mkenda na Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais Tamisemi Mhe. Deo Ndejembi, baada ya kukutana katika hafla ndogo iliyofanyika hoteli ya Kilimanjaro Hyatt jijini Dar es salaam leo asubuhi.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Ushirikiano wa Elimu Duniani (GPE), Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, akiwa na Afisa Mtendaji Mkuu wa GPE, Bibi Laura Frigenti, leo asubuhi wamekutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Elimu Profesa Adolf Mkenda na Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais Tamisemi Mhe. Deo Ndejembi, pamoja na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Dk. Natu El- Maamry Mwamba, Kamishna wa Idara ya Usimamizi wa Madeni wa Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Japhet Justine na Mkurugenzi wa Sera na Mipango Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Bw. Atupele Mwambene katika hafla ndogo iliyofanyika hoteli ya Kilimanjaro Hyatt jijini Dar es salaam.
Mazungumzo hayo, ambayo ni sehemu ya shughuli za viongozi hao wakuu wa Shirika hilo ambalo litakuwa na mkutano wa Bodi ya Wakurugenzi Zanzibar Jumatatu, yalihusu uhusiano mzuri uliopo kati ya GPE na serikali ya Tanzania ambao umedumu kwa miaka 10 sasa ambapo kwa kipindi hicho hadi sasa Shirika hilo ambalo liko chini ya Benki ya Dunia limeishaipatia Tanzania jumla ya Dola za Kimarekani Milioni 332 (takriban shilingi 834,980,332,000.00) ili kusaidia sekta ya elimu bara na visiwani. Juzi November 1, 2023 GPE imetiliana saini na Serikali ya makubaliano ya kutoa dola za Kimarekani milioni 85 (takriban shilingi 213, 775, 085, 000.0) kwa ajili ya kusaidia mafunzo ya walimu nchini.
Picha na Ofisi ya Rais Mstaafu
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...