Na Pamela Mollel,Arusha

Aliyewahi kuwa Mkuu wa Wilaya sehemu mbalimbali nchini na Mwenyekiti wa halmashauri ya Arumeru Mstaafu Thomas Loy Ole Sabaya amechaguliwa kuwa Mwenyekiti Mpya wa chama hicho Mkoa kwa kupata idadi kwa kupata kura 463 huku mpinzani wake wa karibu Daniel Palagyo akipata kura 374 kati ya kura 951 huku Moja ikiharibika.

Uchaguzi huo umekuja kufuatia kifo cha aliyekuwa Mwenyekiti wa chama hicho Mkoa wa Arusha Marehemu Zelothe Stephen aliyefariki octoba 26 Jijini Dar es salaam alipokuwa akipatiwa matibabu.

Akiongea mara baada ya kuchaguliwa Sabaya amesema amewashukuru sana wajumbe akisema CCM hii ndio domokrasia maana kijana wangu amenikimbiza na kuonyesha ukomavu hivyo nitashirikiana na Wanachama wote kuanzia ngazi ya kitongoji kuhakikisha Mradi wa uchaguzi Mkuu unafanikiwa.

Aidha Akabainisha kuwa Arusha tuna bahati kwa kuwa na wajumbe wa kamati kuu 4 na kama hatufanyi mambo yakaenda tutakuwa hatutendi haki kwa kuwa Mkoa huu ni kinara na hatuna sababu ya kulia Lia tujenge Umoja na kuondoa Makundi.

Alisema Tuanza Mradi wa kushinda uchaguzi tukienda katika uchaguzi na makundi hatutashinda tutafute kero za wananchi ili kushinda uchaguzi sitegemea Kuna mtu atakwamishi kama tumepatana na kuondoa Makundi

Nawaahidi kushirikiana na wenzangu wote na wananchi tusikwamishane tunataka kushika Dola tunatakiwa kutatua kero za wananchi ili tushike Dola naomba wote tujiandae kwa uchaguzi

"Sitegemei Kuna namna ya kukwamishana hivyo tuanze Mradi wa kushinda uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi Mkuu twendeni kukipigania chama chetu"

Akiongea wakati akitangaza Matokeo ya uchaguzi huo Msimamizi Mkuu wa uchaguzi huo Anthony Mtaka ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa wa Njombe amesema Sabaya amepata kura 467 huku Dkt.Palangyo akipata kura 374 na Edna Kivuyo kura 10 na Solomon Kivuyo akipata kura 56

Amesema wajumbe 951 wamepiga kura ambapo idadi kamili ya wajumbe waliotakiwa kupiga kura ni 1001 ndipo akamtangaza rasmi Thomas Loy Sabaya kuwa Mwenyekiti wa chama hicho Mkoa wa Arusha.

Amesema kwamba uchaguzi huo uwe sehemu ya kuongeza mshikamano na wajumbe kutambua umuhimu wa uchaguzi na kanuni zake zitakazosaidia kupata kiongozi makini atakayewaongoza na kukisemea chama kuelekea uchaguzi Mkuu.

Mtaka amemtaka Mwenyekiti kushikamanisha Wanaarusha na kuhubiri upendo mshikamano utulivu na amani Arusha wape upendo Wanaarusha waheshimishe unapohubiri yatoke moyoni kujenga Arusha.

Kwa Upande wake Mwenyekiti wa Muda Namelock Sokoine kuwapongeza viongozi karibuni na poleni mwaka Jana tulifanywa uchaguzi tulimchagua Zelothe Stephen kuwa Mwenyekiti lakini Mungu kwa Shani yake amemchukuwa hivyo kamati kuu ilituletea wagombea wa nne nafasi hiyo.

Amesema Tunamshukuru Mwenyekiti wetu Samia na kamati kuu kwa kututeulia wajumbe hawa wataogombea nafasi hii tunaimani Mojawapo atakayechaguliwa hapa atatupitisha katika uchaguzi Mkuu na serikali za mitaa kwa kishindo.

Amesema Uchaguzi huo ukawe alama ya Umoja mshikamano wetu naomba kwa Kauli ya pamoja tunamuunga Mwenyekiti wetu Rais Samia Suluhu Hassan tuungane kwa pamoja tukionyesha Umoja wetu na mshikamano wetu katika uchaguzi huu..

Hata hivyo Katibu wa Mkoa wa CCM Arusha Mussa Matoroka akisoma akidi ya wajumbe wa Mkutano huo amesema Idadi ya wajumbe wa Mkutano huo Arusha Mjini 128 Arumeru 160 longido 115 Meru 161 Karatu 88 Ngorongoro 156 Meru 153 Monduli 124 Mkoa 19 ikiwa idadi kwa ujumla ya wapiga kura 951 kati ya wajumbe 1003.

Nao WASIMAMIZI wa uchaguzi waliombatana na Msimamizi Mkuu Shani Ngatite na Husein Mwaga walitoa angalizo la wajumbe kutoa idadi sahihi ili kutovuruga uchaguzi huo kwani hawatasita kuchukuwa hatua nawafuate kanuni taratibu za uchaguzi ndani ya chama.

Wagombea waliogombea katika Mkutano huo maalumu ni Loy Sabaya Daniel Palagyo,Edna Israel Kivuyo,Solomon Ole Sendeka Kivuyo

Wakati akiomba kura mgombea Edna Kivuyo amesema kuwa suala na makatibu wa CCM kata kulipwa fedha hilo nitaenda kusimamia kuhakikisha wanarudisha utaratibu wa zamani kwa Lengo la kurudisha nidhamu ndani ya chama.

Nae Mgombea Solomoni Kivuyo amesema ataunganisha chama na serikali sanjari na kuleta Umoja kwa kutumia uzoefu wake wa miaka zaidi ya 44 ndani ya serikali.

Awali Mgombea Daniel Palagyo amesema kwamba miaka 10 ya kuwepo ndani ya uongozi wa chama Sasa ameiva kuweza kuwa Mwenyekiti wa Mkoa katika kutatua changamoto za wafugaji wakulima wafanyabiashara wakubwa na wadogo wa Mkoa wa Arusha.

Wagombea wote baada ya kutagazwa Matokeo hayo wamepongeza uchaguzi huo na kuelezea umeenda kwa haki huku wakieleza kutoa ushirikiano kwa Mwenyekiti Huyo Kuendeleza umoja.




 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...