Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi amesema Serikali itaendelea kuimarisha mfumo wa kodi ulio rahisi kuutumia kwa kuwekeza zaidi katika mifumo ya kidijitali na kuwafikia walipa kodi wengi zaidi pamoja na kuimarisha  ofisi za kodi kila Mkoa na Wilaya zake Zanzibar.

Rais Dkt.Mwinyi amesema hayo katika hafla ya Maadhimisho ya mwezi wa Shukrani na Furaha kwa mlipakodi iliyoandaliwa na Mamlaka ya Mapato Zanzibar (ZRA) ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip Airport, Mkoa wa Mjini Magharibi tarehe: 29 Disemba 2023.

Halikadhalika Rais Dkt.Mwinyi amempongeza Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Zanzibar (ZRA) Yusuph Mwenda kwa kuleta mabadiliko ya utendaji na ufanisi wa kuongezeka ukusanyaji mapato Zanzibar  .

Aidha Rais Dkt.Mwinyi ameiagiza  Wizara ya Fedha na Mipango kuhakikisha ZRA inapatiwa bajeti asilimia 100.

Pia ameiagiza Wizara ya Nchi ofisi ya Rais Utumishi kwa kushirikiana na Wizara ya Fedha na Mipango  kukamilisha marekebisho ya stahiki ya mishahara ya watumishi wa ZRA.

Vilevile Rais Dkt.Mwinyi amezindua mfumo mpya wa kusimamia ukusanyaji wa mapato ya kodi ZIDRAS  (Zanzibar Integrated Domestic Revenue Administration System).

Kwa upande mwingine Rais Dkt.Mwinyi amewapongeza wafanyabiashara wote wakubwa, wa kati na wadogo wa Unguja na Pemba walioshinda Tuzo za ulipaji kodi vizuri Zanzibar.








Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...