Na Mwandishi wetu

Shule ya Msingi Lusasaro Iliyoko Tabata Kisukuru imewaomba Watanzania na serikali kwa jumla kumsaidia mtoto yatima Elia Hubert (14) aliyemaliza shuleni hapo.

Mwalimu wa Taaluma wa Shule hiyo Maganiko Simon anasema kwamba shule yake imemsomesha mtoto huyo bure elimu ya msingi na kuweza kufaulu vizuri na kuchaguliwa kujiunga shule ya serikali ya kutwa ya Bagoza ila changamoto ni uwezo duni wa familia yake ambayo haiwezi kumudu gharama za elimu za kijana huyo.

Naiomba serikali impangie shule ya bweni na pia nawaomba watanzania wamchengie kijana fedha za kumuwezesha kumudu gharama mbalimbali za elimu kupitia namba 0756729019 majina ya Mpokeaji Joyce Ngalula.

Naye mama Mlezi wa Kijana huyo Saada Hussein anawaomba watanzania wamchangie kijana huyo ili aweze kumudu gharama za elimu huku akiiomba serikali impangie kijana huyo shule ya bweni kwani familia yake haina uwezo hata wa kumpa nauli na malazi kijana huyo. Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...