Shule ya Nuru Angavu iliyoko Mwanagati, Ilala, Mkoa wa Dar es Salaam  imefanya vizuri Matokeo ya Darasa la saba kwa mwaka 2023 , Ki-mkoa imeshika nafasi ya nane kwa upande wa shule zenye idadi ya watahiniwa chini ya 40 kwa darasa.

Meneja wa shule hiyo ya mchepuo wa Kiingereza Mary Kimaro anasema kuwa siri ya mafanikio ya shule yake ni ushirikiano baina ya wazazi waalimu na mamlaka zinazosimamia elimu hapa nchini.“Bila ushirikiano huo tusaingefikia hapa, utaona umuhimu wa ushirikiano katika kufanikisha jambo lolote lile,” anasema.

Anatoa wito kwa wazazi kuwa maeneo yanayoizunguka shule yao na Jijini la Dar es Salaam kwa ujumla kuhakikisha kwamba wanawapeleka watoto wao shuleni hapo kama wanataka wapate elimu bora.

Anasema shule yake imeomgoza katika Kata yao ya  mzinga na kwamba wamejipanga kufanya vizuri zaidi siku zijazo.Anasema kwamba wamejipanga kukuza vipaji vya vijana iwe katika masomo au katika michezo kwa ujumla kwani vipaji katika Dunia ya sasa vinalipa sana.

Anasema shule yake pia inasomesha vijana 30  bure ambao wanatoka katika familia duni lakini wakiwa na uwezo wa kimasomo.

“Tunasaidia vijana hawa ili kuwawezesha kupata elimu bora hata kama hawana uwezo wa kiuchumi.Anatoa wito kwa taasisi mbalimbali kushirikiana na taasisi yake katika kuwasaidia vijana hao.

Wanafunzi wa Shule ya Mwanagati
Mary Kimaro Meneja wa Shule ya Nuru Angavu ya Mwanagati, Ilala Dar es Salaam


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...