WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Prof.Joyce Ndalichako amesema serikali itaendelea kuthamini mchango na kazi zinazofanywa na sekta binafsi katika kutatua changamoto ya ukosefu wa ajira hapa Nchini.

Ameyasema hayo Desemba 4, 2023 Jijini Dar es salaaam wakati akimwakilisha Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kwenye ugawaji wa Tuzo za Waajiri Bora kwa mwaka 2023  zilizoandaliwa na Chama cha Waajiri Tanzania (ATE).

Ndalichako ameongezea kwa kusema kuwa waajiri wazingatie sheria ya watu wenye ulemavu inayowataka kuwaajiri kwani asilimia 3% kati ya watu 20 iwe ya walemavu .

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa chama cha waajiri Tanzania (ATE) amesema Tangu kuundwa kwa Tuzo hizo za mwajiri bora wa mwaka zimekuwa zikihamasisha makampuni kuweka juhudi katika maswala ya usimamizi wa rasilimali watu kwa kufata sheria , kuweka sera, kanuni na mazingira bora ili kuongeza tija kwa waajiri.

Kwa upande wake Mkurugenzi mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) Hamza S.  Johari waliotwaa tuzo ya pili katika kipengele cha mwajiri bora sekta ya Umma amesema tuzo hiyo ni chachu kwa taasisi yao na itasaidia kuleta chachu na hari kwa taasisi ameongezea kwa kusema wataboresha kitengo cha rasilimali

Tuzo hizo za mwaka ambazo taasisi na makampuni 1500 walionesha nia ya kuwania ila taasisi 91 ndio zilizokidhi viwango kwenye tuzo hizo
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Prof.Joyce Ndalichako Prof. Joyce Ndalichako akimkabidhi cheti cha udhamini kwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) Hamza S. Johari wakati wa hafla ya kutoa tuzo za waajiri bora kwa mwaka 2023 zinazoratibwa na Chama cha Waajiri Tanzania (ATE) ziliyofanyika Desemba 04, 2023 katika ukumbi wa  Mlimani City jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) Hamza Johari (kushto) akionesha tuzo ya mshindi wa pili ya mwajiri bora katika sekta ya umma kwa mwaka 2023 wakati wa hafla ya kutoa tuzo za waajiri bora kwa mwaka 2023 zinazoratibwa na Chama cha Waajiri Tanzania (ATE) ziliyofanyika Desemba 04, 2023 katika ukumbi wa  Mlimani City jijini Dar es Salaam..
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Prof.Joyce Ndalichako akisoma hotuba  kwa niaba ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa wakati wa hafla ya kutoa Tuzo za Waajiri Bora kwa mwaka 2023 zinazoratibwa na Chama cha Waajiri Tanzania (ATE) ziliyofanyika Desemba 04, 2023 katika ukumbi wa  Mlimani City jijini Dar es Salaam.
Mwakilishi wa Benki ya Dunia - Tanzania,Frank Ajilope(kulia) akimkabidhi tuzo ya mshindi wa pili ya mwajiri bora katika sekta ya umma kwa mwaka 2023 Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) Hamza S. Johari (kushoto) wakati wa hafla ya kutoa tuzo za waajiri bora kwa mwaka 2023 zinazoratibwa na Chama cha Waajiri Tanzania (ATE) ziliyofanyika Desemba 04, 2023 katika ukumbi wa  Mlimani City jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) Hamza S. Johari (kushoto) akizungumza jambo wakati wa kumtangaza  mshindi wa tuzo ya kipengele cha ufanisi usimamizi rasilimali watu kwa mwaka 2023 wakati wa hafla ya kutoa tuzo za waajiri bora kwa mwaka 2023 zinazoratibwa na Chama cha Waajiri Tanzania (ATE) ziliyofanyika Desemba 04, 2023 katika ukumbi wa  Mlimani City jijini Dar es Salaam..
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) Hamza S. Johari akimkabidhi Mkurugenzi Rasilimali Watu wa Vodacom Vivienne Penessis (kushoto) Tuzo ya mshindi kipengele cha Ufanisi Usimamizi rasilimali watu kwa mwaka 2023 wakati wa hafla ya kutoa tuzo za waajiri bora kwa mwaka 2023 zinazoratibwa na Chama cha Waajiri Tanzania (ATE) ziliyofanyika Desemba 04, 2023 katika ukumbi wa  Mlimani City jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya Wafanyakazi  wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) wakiongozwa na Mkurugenzi Mkuu Hamza S. Johari wakati wa hafla ya kutoa tuzo za waajiri bora kwa mwaka 2023 zinazoratibwa na Chama cha Waajiri Tanzania (ATE) ziliyofanyika Desemba 04, 2023 katika ukumbi wa  Mlimani City jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Prof. Joyce Ndalichako akiwa kwenye picha ya Pamoja na washindi wa Tuzo za waajiri bora kwa mwaka 2023 wakati wa hafla ya kutoa tuzo hizo zinazoratibwa na Chama cha Waajiri Tanzania (ATE) ziliyofanyika Desemba 04, 2023 katika ukumbi wa  Mlimani City jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) Hamza S. Johari ( wa pili kushoto waliokaa)  akiwa kwenye picha ya pamoja na Mkurugenzi wa Huduma TCAA, Teophory Mbilinyi ( wa kwanza kushoto waliokaa), Meneja Rasilimali Watu na Utawala Amina Silanda Ally (wa pili kulia waliokaa) pamoja na wafanyakazi wa TCAA  wakati wa hafla ya kutoa tuzo za waajiri bora kwa mwaka 2023 zinazoratibwa na Chama cha Waajiri Tanzania (ATE) ziliyofanyika Desemba 04, 2023 katika ukumbi wa  Mlimani City jijini Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...