Na Mwandishi Wetu.
Amesema miongoni mwa kazi hizo za ugunduzi zipo za mfumo wa akili bandia (AI) ikiwemo za umwagiliaji kuzuia upotevu wa maji magonjwa katika mimea ya mazao kuzuia uduma u wa mimea na njia za kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.
Aidha katika tuzo hizo, wanafunzi wa shule ya sekondari ya wavulana ya Bwiru iliyoko mkoani Mwanza waliibuka washindi wa jumla wakiwa na mradi uliotafuta usafi wa maji ya kunywa kwa shule za sekondari.
Mada hiyo inatokana na kuwepo Kwa tatizo la magonjwa ya mara kwa mara ya tumbo, amiba kwa wanafunzi wa shule za bweni , hivyo kuhitaji kujua kiwango cha usafi na usalama wake.
Pamoja na hayo amesema tuzo hizo kwa wanafunzi zinasaidia kuhamasisha masomo ya Sayansi katika kuleta mabadiliko chanya katika jamii.
Amewataka wanafunzi kuendelea kusoma kwa bidii na kuongeza ubunifu katika nyanja mbalimbali kwani ni eneo linaliweza kuonesha vipaji vyao.
Ameeleza kwamba maonesho hayo yanahamasisha masomo ya Sayansi mashuleni katika kuleta mabadiliko nchini.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya YST,Profesa Yunus Mgaya amesema wanafunzi wamekuwa na mawazo ya kisayansi yenye kuwajenga Kwa siku zijazo.
" Ni mawazo yanayofungua fursa mbalimbali za kufikia uluhu za matatizo yaliyopo katika jamii,ambayo ya ajenga kizazi chenye kupata suluhu za kisayansi," amesisitiza.
Wakati huo huo Mfadhili wa wanafunzi wanaoshinda katika tuzo hizo kutoka Karimjee Foundation Vinoo Sumaiya amefafanua kupitia tuzo hizo tayari wanafunzi 41 walishapata udhamini wa kusoma elimu ya vyuo vya elimu ya juu.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...