Mwenyekiti wa Chama cha ACT- Wazalendo Taifa Ndugu Juma Duni Haji amewahimaiza wazanzibari wote kuhakikisha kwamba wanajiandikisha katika Daftari la wapiga kura ili kujeweka tayari kwa kushiriki katika uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025 .

Mwenyekiti huyo ameyasema hayo huko katika viwanja vya Mpira vya Kwabamgeni katika Jimbo la Pangawe ikiwa ni mfululizo wa mwendelezo wa mikutano ya hadhara ya chama hicho kuzungunza na wananchi.

Amsema kwamba wananchi hawapswi kuvunjika moyo kutokana na changamoto mbali mbali zinazojitokeza wakati wa uwandikishaji ikiwemo mashine kutokusoma alama za vidole na badala yake waendelee na jithada ili kuweza kuwa wapiga kura halali.

Amefahamisha kwamba wale wanaovunjika moyo wanapaswa wakumbushwe kwamba kura ni haki yao na kwamba lazima waipate na waitumie haki hiyo kujakuwachagua viongozi wanaowataka wakati utakapowadia.

Aidha wamewakumbusha vijana wote ambao hawanavitambulisho vya mzanzibari mkaazi kuhakikisha kwamba wanafika katika ofisi za msheha kwa ajili ya kupata vitambulisho hivyona kamwe wasivunjike moyo na vikwazo vinavyojitokeza kwa kuwa kuvunjika moyo hakutawafanya kuwa wapiga kura.

Amewataka masheha kuacha tabia ya kuwanyima barua za vitambulisho wananchi kwa kuwa kufanya hivyo ni ubaguzi kwa wananchi huku kitambulisho kikiwa ni haki yakila mwananchi kisheria nakwamba ni kazi yake kutoa barua kwa wananchi wote.

Naye Makamu Mwneyekiti wa Chama hicho ambaye pia ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Othman Masoud Othman, amesema kwamba wazanzibari wanaendea kugubikwa na umasikini jambo linalopaswa lisiendelee kuwepo.

Amesema kwamba kutokana na Zanzibar kutokua na mamlaka hata wafanyabiashara wakubwa hivi sasa wanaendelea kuondosha biashara zao na kuifanya Zanzibar kuwa na hali ngumu kiuchumi jambo ambalo ni wananchi pekee kupitia kura wanaoweza kuliondoa.

Amewahimiza wananchi kuhakikisha kwamba wanapata vitambulisho vya mzanzibari mkaazi na hatimaye waweze kujiandikisha na kuwa wapiga kura halali ili kuweza kuta viongozi wanaoweza kuwajibika na kuwajibishwa na wananchi wenyewe.

Naye Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama hicho Ismail Jussa amesema kwamba chama chake kitaedelea kueleza masuala mbali mbali mbele ya umma ambayo wanaamini kwamba uendeshaji wake hauna manufaa kwa wananchi kama walivyofanya kwenye mikutano ya awamu iliyopita.

Mwisho.

Imetolewa na ofisi ya Makamu wa Kwanza wa rais wa Zanzibar

Kitengo cha Habari

Leo tarehe 16.12.2023.
 

Makamu Mwenyekiti wa  ACT-Wazalendo Mhe. Othmna Masoud akizungunza katika mkutano wa hadhara huko viwanja vya bamgeni jimbo la Pangawe leo tdsemba 16.23

Mwenyekiti wa ACT- Wazalendo Babu Juma Duni akiasalimiana na Makamu wake Mhe, Othman Msoud mara walipowasili jimbo la pangawe kwa mkutano wa hadhara leo disemba 16.23

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...