Na. Damian Kunambi, Njombe

Kijana mmoja mkazi wa kata ya Masasi wilayani Ludewa mkoani Njombe aliyefahamika kwa jina la Michael Haule (35)  amefariki dunia huku Alto Mligo (53) akivunjika mkuu na kujeruhiwa katika eneo la kituani baada ya kuporomokewa na udongo wa kifusi cha kingo za barabara ya Kimelembe ambayo ujenzi wake unaendelea.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo mkuu wa wilaya ya Ludewa Victoria Mwanziva amesema tukio hilo limetokea baada ya gari aina ya Center lenye namba za usajili T974 AXD lililokuwa likiendeshwa na Alto kukwama katika eneo hilo ndipo Michael (marehemu) ambaye alikuwa akiendesha pikipiki aliamua kusaidiana na dereva huyo kulinasua gari hivyo wakiwa katika harakati za kulinasua ndipo kiliposhuka kifusi hicho na kuwafunika.

"Tunasikitishwa sana na taarifa ya ajali hii ya kifusi katika Mlima Kimilembe tunazidi kutoa rai kwa wananchi kuwa makini katika utumiaji wa njia hiyo ambayo ipo kwenye matengenezo hasa katika kipindi hiki cha mvua".

Sanjari na hilo pia Mkuu huyo wa wilaya amesema kwa sasa timu nzima ya Wakala wa barabara Tanzania (TANROAD) mkoa wa Njombe wamefika katika eneo la tukio na wanaendelea na zoezi la kuweka njia sawa ili iweze kuendelea kutumika.
Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...