Na Mwandishi Wetu, Michuzi TV

Balozi Robert Scott ambaye ni Deputy of the Commander for Civil - Military Engagement, United State Africa Command (USAFRICOM))ametembelea ofisi za Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya(DCEA).

Lengo la kuitembelea Mamlaka hiyo ni kuipongeza kutokana na kutambua kazi kubwa inayoifanya baada ya mafanikio ya ukamataji mkubwa uliofanyika nchi ambapo zaidi ya tani tatu za dawa za kulevya zilikamatwa.

Taarifa iliyotolewa leo kwa vyombo vya habari na Mamlaka hiyo imesema ujio wa Balozi Scott katika Mamlaka hiyo pia ni muendelezo wa mashirikiano mazuri yaliyopo kati Tanzania na Marekani katika kupambana na janga lq dawa za kulevya duniani.

Aidha, balozi Scott, kwa niaba ya Mkuu wa Kamandi hiyo General Michael Langley amemkabidhi Kamishna Jenerali Aretas Lyimo cheti kwa kutambua juhudi hizo.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...