MKUU wa Wilaya ya Geita Cornel Magembe amefanya kikao Shule ya Msingi Nyansalala iliyoko Kata ya Bukondo Halmashauri ya Wilaya ya Geita kutokana na taarifa zilizosambaa kwenye mitandao ya kijamii zikionesha walimu wa Shule hiyo wakiwa wamekalia vitabu.

Sababu za kukalia vitabu ni baada ya Mtendaji wa Kijiji kuwanyang'anya walimu hao madawati waliyokuwa wanakalia kwamadai Mwalim Mkuu wa Shule hiyo kuchelewesha kuleta samani hizo kama alivyoahidi katika vikao vya kamati.

Hata hivyo jambo hilo limeshapatiwa majibu baada ya samani hizo kufikishwa katika shule hiyo na hiyo baada ya mzabuni aliyepewa kazi hiyo kutokukamilisha kwa wakati kama ambavyo makubaliano yalifanyika katika mkataba kati ya shule na mzabuni.

Shule hiyo ina jumla ya walimu 12 na wanafunzi 1179. Kwa sasa Walimu wa Shule hiyo wanaendelea na majukumu yao baada ya meza 8 na viti 8 kupelekwa shuleni hapo.

Katika kikao hicho kilihudhuriwa na viongozi wa ngazi mbalimbali katika halmashauri hiyo ,walimu wa shule ya Msingi Nyansalala, viongozi wa CCM ngazi ya Kata, Mwenyekiti wa Chama Cha Walimu Geita, maofisa elimu Kata pamona na uongozi wa Serikali ya Kijijini.




 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...