MKUU wa Wilaya ya Kilosa mkoani Morogoro Shaka Hamdu Shaka ameagiza viongozi wa kata ya Parakuyo kuanza msako kutafuta walipo wanafunzi 54 wa kidato cha kwanza walioshindwa kuripoti kwa wakati katika shule ya Sekondari Parakuyo, walipopangwa jumla ya wanafunzi 59 ambapo mpaka sasa ni wanafunzi watano pekee waliokwisha ripoti.
Ametoa agizo hilo alipo tembelea shule hiyo ya sekondari Parakuyo, Kata ambayo zaidi ya asilimia 95 ya wakazi wake ni wafugaji jamii ya kimasai, akisema ipo tabia ya baadhi ya wazazi na walezi kuacha kuwapeleka watoto wao kwenye shule walizo pangiwa badala yake kusingizia kutaka kuwahamishia kwenye shule binafsi kisha baadhi yao kutumia mwanya huo kuwaozesha.
Ikumbukwe kuwa kwa wilaya ya kilosa pekee kuna jumla ya wanafunzi 10,063 waliopangwa kuanza kidato cha kwanza mwaka huu 2024, miongoni mwa wanafunzi 14, 371 waliofanya mtihani wa mwisho wa kuhitimu elimu ya msingi mwaka 2023.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...