Na Ashrack Miraji Same kilimanjaro
DIWANI wa Kata ya Same Mjini mkoani Kilimanjaro Mritha Emezitaka Shule ambazo zipo kwenye kata yake kuhakikisha zinapika chakula Bora Kwa wanafunzi wanaosoma shule hizo
Mritha ameyasema hayo akiwa katika ziara za kukagua miradi mbalimbali ndani ya Kata yake ambapo alitembelea Shule ya Msingi N.A iliyopo Wilaya ya Same mkoani kilimanjaro kukagua idadi ya wanafunzi waliofika shuleni na ubora wa chakula kinachoandaliwa shuleni kwa ajiri ya wanafunzi
"Nikutoe rai kwa wazazi wenzangu wenye watoto kwenye shule yoyote iliyopo katika Kata yoyote kuhakikisha watoto wao wanakula mashuleni kwani nijukumu la mzazi kuhakikisha mwanae anapata milo mitatu kwa siku kwa mujibu wa sheria, "amesema
Ameongeza kuwa "Kuna baraka ya kipekee sana kwa mzazi hata kwenye shuhuli zako za mihangaiko mwanao anapokuwa amekula na kushiba tena kwa jasho lako.Ikumbwe kwa mzazi kufanya jukumu lake hilo litaleta chachu kwenye matokeo ya watoto wetu."
Pia Diwan Mritha amesema wao Madiwani wanajukumu zito la kumsaidia Rais Dk.Samia Suluhu Hassani kwa Kazi kubwa anayoifanya Katika kuleta Maendeleo kwenye Taifa ni Mama ambaye anajua uchungu wa watoto wetu .
Akizungumzia kuhusu yaliyofanywa na Rais Dk.Samia wilayani Same , amesema Rais Samia ameyafanya mambo makubwa yakiwemo ya ujenzi wa shule nyingi ndani ya Wilaya hiyo.
"Tunamshukuru Rais Samia kwa kutuletea fedha kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maendeleo, amefanya mambo makubwa kwa kushirikiana na Mbunge wetu wa Jimbo la Same Magharibi David Mathayo ambaye amekuwa akipambana kuhakikisha jimbo letu linakuwa na maendeleo."
Amewaomba wananchi wa Same kuendelee kumuunga mkono Rais Dk. Samia Suluhu Hassani pamoja na Mbunge wao kwani wamekuwa wakifanya kazi kubwa na nzuri ya kuhakikisha maendeleo yanapatikana.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...