Njombe
Wakulima wa wilaya ya Ludewa mkoani Njombe wameingiwa na hofu ya janga la njaa kutokana na wadudu aina ya Viwavi jeshi kuvamia katika mashamba yao na kushambulia mazao ambapo wameiomba serikali kuchukua hatua za haraka kuwadhibiti wadudu hao ili wasiweze kuleta athari zaidi.
"Hawa wadudu wameshambulia maeneo ya watu na Mahindi ya watu ambapo waligharamia mbegu,tunaomba serikali itoe msaada wa Helikopta ili itumie kumwaga dawa kuua hawa wadudu"amesema Francis Mwinuka
Ayo TV imezungumza na afisa kilimo wa wilaya hiyo Godfrey Mlelwa ambaye amethibitisha juu ya uwepo wa wadudu hao ambapo amesema mpaka sasa maeneo yaliyo athirika zaidi ni maeneo ya Nyamapinda na Mdonga yaliyopo kata ya Ludewa ambapo zaidi ya ekari 380 za mashamba yaliyolimwa na yasiyolimwa yamevamiwa na wadudu hao.
"Jumla ya ekari 380 zimevamiwa na hao wadudu na kati ya hizo,ekari 280 zilikuwa ni eneo la mazao ya Mahindi na ekari 100 ni eneo la mapori ambalo limeachwa wazi na eneo jingine la ekari kama 100 ni la wenzetu wa taasisi ya Magereza"
Aidha amesema tayari serikali imekwisa anza kuchukua hatua ambapo wizara ya kilimo kupitia taasisi inayojihusisha na afya ya mimea (TPHPA) imeweza kutoa dawa Lita 1,000 ili kupambana na Wadudu hao ambapo mpaka sasa tayari lita 185 kati ya hizo zimekwisha tumika.
.jpeg)

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...