Na Mwandishi Wetu

Wakazi wa Ukonga, Wilaya ya Ilala Jijini Dar es Salaam wametakiwa kupeleka watoto wao shuleni Gisela kwa elimu bora.

Mkuu wa Shule ya Msingi Gisela ambayo ni ya Mchepuo wa Kiingereza, Malimi Kwilasa anasema kuwa shule hiyo imekuwa ikifaulisha kila mwaka kwa wastani mzuri wa A na hivyo kuifanya kuwa moja ya shule bora Wilaya ya Ilala.

Pia shule hiyo ina shule ya awali au chekechea.

Anasema matokeo ya mwaka jana darasa la saba shule ilikuwa na watahiniwa 92 kati yao waliofaulu kwa daraja la A ni 85 wakati daraja B ni saba tu.

“Hivyo kwa mantiki hiyo utaona namna shule yetu inayofaulisha, wazazi wawalete watoto wao shuleni hapa” anasema

Anasema wakazi wa tarafa ya Ukonga kata ya Kipunguni wana fursa ya kupeleka watoto shuleni hapo ili wapate elimu bora, shule iko Mtaa wa Amani , barabara ya Bombambili.

Mwalimu Kwilasa anasema kuwa mazingira ya kufundishia ni bora na shule ina usafiri kwa wanafunzi wa maeneo mbalimbali ya Ukonga na hata nje ya Ukonga.
Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi ya Mchepuo wa Kiingereza ya Gisela Malimi Kwilasa.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...