Kampuni ya Xiaomi inayojihusisha na utengenezaji wa vifaa vya kielektroniki zikiwemo simu za mkononi imetaja bei ya simu zake mpya za Redmi Note 13 hapa nchini zilizozinduliwa nchini Thailand hivi karibuni.
Xiaomi imesema imekuja na matoleo tofauti ya simu hizo ili kuwafanya wateja wake wa madaraja yote kuwa na uwezo wa kumiliki simu hizo.
"Redmi Note 13, 6 (128GB) inauzwa Sh469,000, Redmi Note 13, 6 Plus (128GB) Sh509,000 na Redmi Note 13, 8 Plus (256GB) ni Sh559,000," imesema
Nyingine ni Redmi Note 13 Pro 8 Plus (256GB) ambayo inauzwa Sh719,000, Redmi Note 13 Pro 12 Plus (512GB) ni Sh849,000.
Kwa upande wa simu zenye kasi ya 5G ni Redmi Note 13 Pro 8 Plus (256GB) inayouzwa Sh1,029,000 huku Redmi Note 13 Pro 12 Plus (252GB) ikiuzwa
1,159,000.
Matoleo hayo ya Redmi Note 13 yanakuja katika rangi tofauti zikiwemo nyeusi, nyeupe na zambarau, kijani na bluu.
Pia maboresho makubwa kwenye kwenye mifumo wa kamera na betri (5000mAh) zenye uwezo wa kuhifadhi nishati kwa muda mrefu.
Maboresho mengine kwenye matoleo hayo ni pamoja na uboreshaji wa mifumo ya utendaji kazi wa simu unaozipa uwezo wa kufanya kazi kwa kasi bila kukwama-kwama.
Redmi Note 13 zina vioo vyenye picha ang’avu lakini pia zina chaguo la kutumia mwanga wenye kulinda macho huku zikiwa na muonekano mzuri wa nje na zinazovutia watumiaji.
Katika uzinduzi simu huko Thailand Xiaomi pia ilitambulisha saa zake ambazo zina uwezo wa kuunganisha mawasiliano katika simu zake. Saa hizo ni Redmi Watch 4, Redmi Buds 5 Pro na Redmi Buds 5.
Saa hizo za kisasa zinamfanya mtumiaji wa simu kuwa na uwezo wa kupokea simu na kusoma jumbe zinazoingia kwenye simu bila kushika simu.
Pia zina uwezo wa kupima mapigo ya moyo pamoja na oxyjeni kwenye damu ikiwa ni pamoja na kuonyesha muda ambao mtumiaji amesimama au kukaa na kumshauri kukaa kama amesimama kwa muda mrefu na kusimama kama amekaa kwa muda mrefu.
Redmi imewataka wateja wake kutembelea tovuti yake rasmi ili kufahamu mambo mbalimbali kuhusu bidhaa zake na kuepuka utapeli wa bei na bidhaa zisizo na viwango.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...