JUMLA ya ekari 100 kutoka Jeshi la Magereza kwenye eneo la Warret, Wilayani Hanang zimetolewa kwa ajili ya waathirika.

Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Geophrey Pinda ametembelea na kukagua eneo hilo lililotolewa na Jeshi la Magereza ambapo tayari eneo hilo limepimwa viwanja kwa ajili ya kuwahamisha waathirika wa mafuriko yaliyotokana na maporomoko ya mawe na tope kutoka mlima Hanang.

Pinda amefanya ukaguzi huo akiambatana na Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Queen Sendiga pamoja na viongozi wengine wa mkoa pamoja na wa wilaya ya Hanang.

Desemba 21, 2023 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), Jenister Mhagama alielekeza Wizara ya Ardhi kuhakikisha viwanja kwa ajili ya kuhamisha waarhirika maeneo ya Gendavi, Jorodom, Ganana na Katesh - Hanang vinapimwa na kukamilika kabla ya Desemba 31, 2023.


 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...