Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Ndugu Dkt. Emmanuel John Nchimbi, akiendesha Kikao cha Sekreterieti ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC), iliyofanyika leo Jumanne, Januari 16, 2024, Ofisi Kuu ya CCM Zanzibar, iliyoko Kisiwandui, Unguja, ikiwa ni siku moja baada ya kuteuliwa na NEC ya CCM Taifa kushika nafasi hiyo ya Mtendaji Mkuu wa Chama, ambapo baada ya kukaribishwa ofisini na kutia saini, alipata wasaa pia wa kufanya mazungumzo na Manaibu Katibu Mkuu wa CCM, Ndugu Anamringi Macha (Bara) na Ndugu Mohammed Said Mohammed Dimwa (Zanzibar).




 

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Ndugu Dkt. Emmanuel John Nchimbi, akiwasili Ofisi Kuu ya CCM Zanzibar, iliyopo Kisiwandui, Unguja, leo Jumanne, Januari 16, 2024, tayari kuendelea na kazi, siku moja baada ya kuteuliwa na Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC) kushika nafasi hiyo ya Mtendaji Mkuu wa Chama, ambapo baada ya kukaribishwa na Manaibu Katibu Mkuu, Ndugu Anamringi Macha (Bara) na Ndugu Mohammed Said Mohammed Dimwa (Zanzibar) na kutia saini, ameendesha Kikao cha Sekreterieti ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, iliyofanyika ofisini hapo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...