Mapema leo Mbunge w Jimbo la Morogoro Mjini Mhe.Dokta Abdulaziz Abood amefanya ziara ya kushutukiza kwenye Kata ya mazimbu lengo ikiwa ni kujionea miundombinu ya barabara namna ilivyo kwa kipindi hiki cha mvua.
Akiwa maeneo ya balakuda kwenye Kata ya Mazimbu amejionea ubovu wa barabara hiyo inayoelekea chuo Kikuu Cha SUA Kampasi ya Mazimbu namna ilivyoaribiwa na mvua zinazoendele Sababu za kuaribika kwa barabara hiyo ni maji yanayopita mto ngerengere kuacha mkondo wake na kukatisha kwenye barabara hiyo. Jambo ambalo linasababisha watumiaji wa barabara hiyo kuvuka kwa shida na jambo la hatari kwa afya za wananchi.
Mhe Mbunge ameahidi kuongea na TARURA ili kufanya haraka kurekebisha barabara hiyo na kuzuia maji kukatisha sambamba na uchimbaji wa mitaro.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...