Huku ikiwa imebaki takriban mwezi mmoja kabla ya mbio maarufu za Kilimanjaro International Marathon 2024 kufanyika Mjini Moshi, mdhamini mkuu wa mbio hizo, Kilimanjaro Premium Lager ametoa wito kwa washiriki wote wakamilishe maandalizi kwani siku zimebaki chache.

Akizungumza Jijini Dar es Salaam, Meneja wa chapa ya Kilimanjaro Premium Lager, Catherine Lyakurwa alisema siku zimebaki chache hivyo washiriki hasa wale wa mbio za Km 42 hawana budi kujiandaa vizuri.

“Hii ni mbio ndefu ambayo inahitaji mshiriki ajiandae vizuri. Tunafanamu kuwa washiriki wamekuwa wakifanya mazoezi na sasa tuna takriban mwezi mmoja tu ni vizuri tukamilishe maandalizi mapema tayari kwa mbio hizi,” alisema.

Alisema mbio za Km 42 zimejizolea umaarufu mkubwa siku za hivi karibuni huku washiriki wakiongezeka mwaka hadi mwaka.“Namba za kukimbilia zinakaribia kuisha kwa hivyo natoa wito kwa wale ambao hawajajisajili wafanye hivyo mara moja kwani zoezi litafungwa mara tu nafasi zikijaa,” alisema.

Alisema bia ya Kilimanjaro Premium Lager itaendelea kufanya kazi kwa karibu na wadhamini wenza na waandaaji ili kuhakikisha mbio za mwaka huu zinafanikiwa na kuacha kumbukumbu ya aina yake. “Tumekuwa wadhamini wa mbio hizi tangu kuanzishwa kwake miaka 22 iliyopita kutokana na mbio hizi kuwa na faida kubwa kwa biashara yetu na kwa nchi kwa ujumla,” alisema.  

Meneja huyo pia alitoa wito kwa wadhamini wenza kujiandaa na corporate challenge ambapo wadhamini mbalimbali huandikkisha washiriki wao katika mbio mbalimbali  kisha waandaaji hutumia wastani wa mida yao ya kumaliza mbio ili kubaini mshindi wa kwanza, wa pili na wa tatu.

Aliwashukuru wadhamini wenza kwa ushirikiano mkubwa kwani bila ushirikiano kati ya wadhamini na waandaaji mbio hizo zisingekuwa na maganikio makubwa.

Katika hatua nyingine, waandaaji wa mbio hizo wamesisitiza kuwa zoezi la usaiili litafungwa mara tu nafasi zitakapojaa kw ambio husika. Taarifa ya waandaaji hao ilisema bado kuna nafasi chache tu za km 42 na 21. “Nafasi hizi zikijaa tutalazimika kufunga zoezi la usajili kwa mbio husika na kuanza kujiandaa na zoezi la kugawa namba mapema mwezi ujao,” ilisema taarifa hiyo   

Washiriki wanaweza kujisajili kwa kutumia tigopesa kwa kubonyeza *150*01#, kisha bonyeza 5 LKS, kisha bonyeza 5 (Ticket) na kisha ufuate maelekezo ili kukamilisha usajili. Washiriki pia wanaweza kujisajili kwa kupitia tovuti ya www.kilimanjaromarathon.com.

Waandaaji hao walisema kufunga usajili mapema kunasaidia katika maandalizi kama inavyotakiwa na chama cha riadha duniani (WA) ili kuhakikisha usalama wa washiriki na kwamba waandaaji wanaweza kuandaa mahitaji muhimu kama maji na matunda kwa wakati.

Wadhamini wa tukio la mwaka huu ni Kilimanjaro Premium Lager- 42 km, Tigo- 21 km Half Marathon, Gee Soseji – 5Km Fun Run. Wadhamini wa meza za maji ni Simba Cement, Kilimanjaro Water, TPC Sugar, TotalEnergies na CRDB Bank. Wabia rasmi ni –KiliMedair, Garda World Security, CMC Automobiles, Sal Salinero Hotel na wasambazaji wakuu ni – Kibo Palace Hotel na Keys Hotel

Mbio za mwaka huu zitafanyika Jumapili Februari 25 katika Chuo Kikuu Cha Ushirika na kuhusisha mbio za Km 42, 21 na 5.

Kilimanjaro Premium Lager Marathon huandaliwa na Kilimanjaro Marathon Company Limited na kuratibiwa kitaifa na kampuni ya Executive Solutions limited.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...