Na Victor Masangu, Vigwaza.


TAASISI ya Lions Club inayojishughulisha na masuala mbali mbali  ya kijamii imekabidhi tenki nane za kuhifadhia maji katika shule zilizopo kata ya Vigwaza Halmashauri ya Chalinze wilayani Bagamoyo mkoani Pwani.

atanki hayo yanakwenda kusaidia kutunza maji safi na salama kwa ajili ya wanafunzi wakiwa shuleni na kuondokana na adha ya watoto kubeba maji pindi yanapokuwa yamekatika.

Akizungumza kwa niaba ya Mwenyekiti wa Lions Host Kaniz Naghavi,  MuntazirBharwani amesema wametoa tanki hizo pamoja na vyakula baada ya kupokea maombi kutoka kwa Diwani wa Kata ya Vigwaza Mussa Gama.

Amewaomba wakazi wa Vigwaza kuhifadhi na kuyatumia vizuri matanki hayo ili yaweze kuwasaidia wanafunzi na kuwaondoa katika tatizo la kukosa maji wakiwa shule.

"Lions Clubs imepata ufadhili huu kutoka kwenye kampuni ya Refuelling Solutions (T) Limited na wadau wengine na wanachama wa taasisi hii wamechangia kuleta vyakula kwa watoto yatima Vigwaza," amesema.

Taasisi hiyo imetoa hamasa kwa taasisi nyingine kutoa huduma na misaada kwa wanafunzi  wa Shule za hapa nchini kutokana na uhitaji wa vitu vingi utaratibu ambao utasaidia kuboresha masuala ya elimu, afya na michezo.

Gavana wa taasisi hiyo  Hapiness Nkya amesema kwa sasa wapo wanachama 620 na club 23 huku 14 zikiwa Dar es Salaam wamekuwa wakitoa misaada kwenye maeneo mbalimbali ambayo wanashiriki moja kwa moja na mingine kuomba kwenye makampuni.

Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Chalinze Ramadhani Poss, Ofisa Elimu awali na Msingi wa halmashauri hiyo ameishukuru Lions Club kwa misaada ambayo inaitoa kupunguza vikwazo kwa wakazi wa Vigwaza.

Diwani wa Vigwaza Mussa Gama ameishukuru Taasisi hiyo huku akieleza kwamba umekuwa ikisaidia mambo mbalimbali ya maendeleo katika Kata hiyo kwa kutoa vifaa kwenye Zahanati, daftari kwa wanafunzi na sasa matenki na vyakula kwa yatima.

" Hawa Lions wamekuwa ni watu wa karibu wanaomsaidia kutafuta matatizo kwenye kata yetu naomba wadau wengine wajitokeza kutupatia misaada ya fedha na vitu kwenye sekta za afya na elimu," amesema Gama.

 Wakati huo huo Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Ruvu Darajani Samwel Mjema amesema matanki hayo yanakwenda kuwasaidia kutunza maji pindi yanapokatika huku akiahidi kuyatunza Ili yadumu kwa muda mrefu na kuwa msaada kwa wanafunzi.

Shule nane zilizonufaika na matanki hayo ni pamoja na Msilale, Chamakweza,Sekibwa, Ruvu, Kitonga na Kwazoka zote za Msingi na Sekondari ni Mnindi na Ruvu na hivi karibuni matanki mengine mawili yataletwa na kukabidhi a shule husika.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...