MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Abdulurhman Kinana amesema hakuna dhambi kwa kiongozi aliyeko madarakani anapomaliza awamu ya kwanza kupewa awamu ya pili aendelee kuongoza.
Kauli ya Kinana inatokana na ombi la Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ambaye pia ni Mbunge wa Ruangwa na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Kassim Majaliwa kushauri Kamati Kuu na Halmashauri Kuu ziridhie kutoa fomu moja ya urais katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2025 na fomu hiyo ni ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan.

Aliogeza kuwa Rais Samia anaonesha njia kwa kupanga, kutafuta mikakati na kuweka vipaumbele na sasa Watanzania wanajivunia mafanikio na hata wana CCM wanaposema mgombea tuliyenaye anatosha kugombea mwaka 2025 nadhani kama wanasababu yoyote zaidi ya kutambua mchango wake mkubwa katika taifa hili.
“Na Wana-CCM si dhambi kusema fomu ya mgombea urais ni moja kama wanaridhika na kiongozi aliyeko madarakani. Pia CCM tuna utaratibu wetu kiongozi akichukua awamu ya kwanza anapewa kuongoza na awamu ya pili.
“Rais Samia Suluhu Hassan yuko awamu ya kwanza, kwa nini asipewe awamu ya pili? Hakuna sababu ya kusema hapana. Kwa CCM kusema tumezingatia utaratibu wa chama chetu Rais anapomaliza kuongoza awamu ya kwanza anaingia ya pili.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...