Makamu wa Rais ametoa wito huo wakati akifungua Skuli ya Msingi ya Elimu Mjumuisho Jendele iliyopo Wilaya ya Kati, Unguja ikiwa ni shamrashamra za Maadhimisho ya Miaka 60 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
Amesema ni vema watoto hao wakapata elimu ili kuweza kutumia vipaji walivyonavyo kwani serikali imeendelea kuboresha miundombinu ya kujifunzia ikiwemo ya shule jumuishi.
Makamu wa Rais amesema Rasilimaliwatu ni nyenzo muhimu katika kuleta maendeleo ya kijamii na kiuchumi nchini ambapo elimu bora ndiyo inayowezesha uendelezaji wa rasilimaliwatu ili kuchangia kikamilifu katika kujenga Taifa na kuleta maendeleo kwa ujumla.
Amesema sekta ya elimu ni kipaumbele cha Serikali zote mbili zinazoongozwa na Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan na Mheshimiwa Dkt. Hussein Ali Mwinyi ili kujenga jamii iliyoelimika na yenye maarifa muhimu.
Aidha Makamu wa Rais ameongeza kwamba katika Miaka 60 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar ni vema kujivunia hatua kubwa ya Maendeleo iliyofikiwa katika sekta mbalimbali hususani elimu kama vile kuongezeka na kuboreshwa kwa miundombinu ya elimu katika ngazi zote, kuongezeka kwa idadi ya wanafunzi kutoka 25,432 mwaka 1964 hadi kufikia wanafunzi 592,781 mwaka 2023.
Halikadhalika Makamu wa Rais amewasihi wananchi kutambua jukumu la kulinda na kudumisha Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar kwa kukemea vitendo vyovyote vinavyokwenda kinyume na dhamira hiyo.
Amewaasa kufanya kazi kwa bidii ili kujiletea maendeleo ya kila mmoja na Taifa kwa ujumla pamoja na vitendo vyovyote vinavyoweza kuchochea ama kuleta utengano.
Kwa upande wake Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Lela Muhammed Mussa amesema kukamilika kwa mradi huo ni jitihada mbalimbali zinazofanywa na serikali ili kuhakikisha elimu inapatikana katika mazingira mazuri. amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imekusudia kufanya mapinduzi makubwa ya kielimu ambapo yanajumuisha uboreshaji wa miundombinu, kuongeza maslahi ya walimu pamoja na kuongeza vifaa vya kisasa katika vituo vya kutolea elimu.
Amesema katika miaka mitatu ya uongozi wa Rais Dkt. Hussein Mwinyi Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali imefikia lengo la asilimia 150 katika utekelezaji wa uboreshaji wa miundombinu ya elimu.
Skuli ya Msingi ya Elimu Mjumuisho Jendele imegharimu shilingi bilioni 3.7.
Imetolewa na
Ofisi ya Makamu wa Rais
11 Januari 2024.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akisalimiana na viongozi mbalimbali wakati alipowasili katika ufunguzi wa Skuli ya Msingi ya Elimu Mjumuisho Jendele iliyopo Wilaya ya Kati, Unguja ikiwa ni shamrashamra za Maadhimisho ya Miaka 60 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar. Tarehe 11 Januari 2024.

Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akikata utepe
kuashiria Ufunguzi wa Skuli ya Msingi ya Elimu Mjumuisho Jendele iliyopo Wilaya
ya Kati, Unguja ikiwa ni shamrashamra za Maadhimisho ya Miaka 60 ya Mapinduzi
Matukufu ya Zanzibar. Tarehe 11 Januari 2024.

Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akisikiliza
maelezo kutoka kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar
Khamis Abdulla Said wakati akikagua miundombinu mbalimbali katika Skuli ya Msingi
ya Elimu Mjumuisho Jendele iliyopo Wilaya ya Kati, Unguja mara baada ya
kuizindua ikiwa ni shamrashamra za Maadhimisho ya Miaka 60 ya Mapinduzi
Matukufu ya Zanzibar. Tarehe 11 Januari 2024.

Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akiwa katika
picha ya pamoja na wanafunzi wasioona wakati wa ufunguzi wa Skuli ya Msingi ya Elimu
Mjumuisho Jendele iliyopo Wilaya ya Kati, Unguja ikiwa ni shamrashamra za
Maadhimisho ya Miaka 60 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar. Tarehe 11 Januari
2024.

Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akihutubia
wakati wa hafla ya ufunguzi wa Skuli ya Msingi ya Elimu Mjumuisho Jendele
iliyopo Wilaya ya Kati, Unguja ikiwa ni shamrashamra za Maadhimisho ya Miaka 60
ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar. Tarehe 11 Januari 2024.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...