MFUKO
wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), umeendelea kutoa elimu ya
Hifadhi ya Jamii kwenye Maonesho ya 10 ya Biashara ya Kimataifa ya Zanzibar
yanayoendelea kwenye viwanja vya Nyamanzi, Wilaya ya Magaharbi Kisiwani Unguja.
Maonesho
hayo yamezinduliwa Januari 10, 2024 na Raisi wa Zanzibar na Mwenyekiti wa
Baraza la Mapinduzi Mhe.Dkt.Hussein Mwinyi, yakiwa ni sehemu ya Sherehe za
Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
Maonesho
hayo ambayo yamebeba kauli mbiu isemayo “Biashara Mtandao kwa Maendeleo ya
Biashara na Uwekezaji” yanawashiriki zaidi ya 500 kutoka taasisi mbalimbali za
bara na visiwani, wakiwemo wajasiriamali na yanatarajiwa kufikia kilele Januari
19, 2024.
PSSSF
imetumia fursa hiyo kuwahudumia wananchama wake ikiwa ni pamoja na kuwapa elimu
ya matumizi ya teknolojia katika kupata huduma za Mfuko, kupitia PSSSF
Kiganjani.
Huduma
hizo ni pamoja na kupata taarifa za Mafao yatolewayo na Mfuko, Taarifa za
Michango, Taarifa za Uwekezaji ikiwa ni pamoja na Wastaafu kujihakiki.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...