KAMPUNI ya Queen J Investment imehimiza wasichana kujitokeza kwa wingi kujiandikisha kwa ajili ya kushiriki Miss Kinondoni 2024.

Akizungumza kwenye uzinduzi wa Miss Kinondoni Jijini Dar es Salaam Mkurugenzi wa Kampuni hiyo Queen Johnson amesema fainali za shindano hilo zitafanyika Mei 11 mwaka huu kusaka washindi watakaowakilisha kwenye taji la urembo la Taifa.

"Tumefungua rasmi pazia kwa wasichana wanaotaka kuwania taji la urembo Kinondoni wajitokeze kujiandikisha ili kuingia kwenye kinyang'anyiro cha kuwania taji la urembo."

Amefunguka na kusema kwa muda mrefu wamekuwa ni wadau wa shindano la Miss Tanzania na kuwashukuru Kampuni ya The Look Kwa kuwapa jukumu mwaka huu kuandaa shindano hilo kwa mara ya kwanza.

Nae Afisa Mwandamizi wa Baraza la Sanaa la Taifa (Basata) Agustino Makame amefafanua kuwa mashindano hayo ni fursa kubwa kwa wasichana na serikali inayatambua kwani yamekuwa yakitoa watu wengi mashuhuri na viongozi.

Pia ametoa rai kwa wasichana wenye sifa za kuwania taji hilo kuchangamkia fursa huku pia, akihimiza wadau, makampuni wajitokeze kwa wingi kuwasapoti waandaaji hao ili kufanikisha.

Kinondoni ina historia ya kutoa warembo katika taji la Miss Tanzania kwa vipindi tofauti na miongoni mwao ni Wema Sepetu mwaka 2006, Nancy Sumari mwaka 2005, Faraja Kota 2004, Richa Adhia mwaka 2007, 2018 Queen Elizabeth na wengine wengi.
Mgeni rasmi Afisa Mwandamizi kutoka Baraza la Sanaa Taifa (BASATA) Agustino Makame akisikiliza kwa makini hotuba ya Mratibu wa shindano hilo Queen Johnson wakati wa uzinduzi wa shindano hilo Jijini Dar es Salaam
 

Wageni mbalimbali waliohudhuria akiwemo Mratibu wa Miss Temeke Tom chilala,Miss Darzone 2023 na Miss Tanzania mshindi wa pili Amina Jigge akiwa na warembo wengine katika Uzinduzi wa Miss Kinondoni Jijini Dar es Salaam
 

Mkurugenzi wa Kampuni ya Queen J Investment  Queen Johnson akizungumza na Wanahabari na Wadau wa Urembo waliojitokeza katika Uzinduzi wa Miss Kinondoni Jijini Dar es Salaam ambapo amewaomba warembo kujitokeza kwa wingi kuchuku fomu ya Mashindano hayo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...