Na Mwamvua Mwinyi, Pwani
Mkuu
wa Mkoa wa Pwani ,Abubakar Kunenge amefafanua kuwa, Mkoa huo una
malengo ya kuandikisha wanafunzi wa shule za awali 55,771 pamoja na
wanafunzi 51,446 wa darasa la kwanza.
Ameeeleza, hadi kufikia mwishoni mwa mwaka 2023 Jumla ya wanafunzi 25,136 wameandikishwa ikiwa ni sawa na asilimia 45.1 .
Akitoa
taarifa hiyo katika kikao cha mtandao cha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais
Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI ambapo alisema mkoa huo,
una malengo wa kuandikisha wanafunzi wa darasa la kwanza 51,446 ambapo
hadi sasa wanafunzi 37,694 wameshaandikishwa, sawa na asilimia 73.3 .
Alieleza, uandikishaji wa shule za awali na darasa la kwanza unaendelea hadi kufikia mwezi Machi mwaka 2024.
Vilevile
akibainisha kuhusu wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha
kwanza mwaka 2024, alisema kwa shule za kutwa na shule Teule ya Mkoa ni
40,796 na ufaulu ukiwa ni asilimia 83.7.
Kunenge
alieleza, wanafunzi wote waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza
wataendelelea na masomo yao bila ya kikwazo chochote.
Kwa
upande wa Miundombinu, Kunenge alieleza, mkoa umepokea jumla ya sh.
Bilioni 29.7 kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu mbalimbali katika sekta
ya elimu.
"Ujenzi
wa shule mpya 36 ,Vyumba vya madarasa 198,nyumba za walimu 13 matundu
ya vyoo 269 ,mabweni 21 vituo vya walimu TRC 13 zitajengwa" Fedha hizi
zimekuja kupitia miradi ya Boost, Sequip one na two kutoka Serikali Kuu,
Barrick na wadau wengine"
Kuhusu miradi ya Boost ,Kunenge alisema mkoa ulitakiwa kujenga shule 13 ambapo baadhi ya shule zimekamilika .
Kwa
upande wa miradi ya Sequip shule zipo 23 na shule 19 kati ya hizo
zimesajiliwa na shule nne zinatarajiwa kusajiliwa mwishoni mwa Januari
2024.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...