Mkurugenzi wa Huduma za Mamlaka Teophory Mbilinyi  ametembelea banda la Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) ambapo amepata maelezo kuhusu Chuo cha Usafiri wa Anga Tanzania (CATC) pamoja na kutembelea mabanda mbalimbali katika maonesho ambayo ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 60 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar yanayofanyika katika viwanja vya Fumba, Zanzibar.

Kwa upande wake Bw. Mbilinyi ameipongeza timu ya maonesho ya TCAA kwa kujipanga vyema na kutoa elimu stahiki kwa wananchi na wadau mbalimbali wanaotembelea banda hilo.

Bw. Mbilinyi amemuwakilisha Mkurugenzi Mkuu wa TCAA Bw. Hamza Johari katika sherehe za Miaka 60 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
Mkurugenzi wa Huduma za Mamlaka Teophory Mbilinyi  akipata maelezo kutoka kwa Mkuu wa Kitengo cha huduma za Viwanja Vya Ndege kutoka Chuo cha Usafiri wa Anga (CATC) Thamarat Abeid kuhusu kozi zinazotolewa na Chuo cha Usafiri wa Anga (CATC) katika Banda la Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania(TCAA) kwenye Maonesho ya Maadhimisho ya miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar yanayofanyika katika viwanja vya Fumba, Zanzibar
Mkurugenzi wa Huduma za Mamlaka Teophory Mbilinyi  akisaini kitabu mara baada ya kupata maelezo ya kazi zinazofanywa na Mamlaka hiyo katika Banda la Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania(TCAA)  kwenye Maonesho ya Maadhimisho ya miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar yanayofanyika katika viwanja vya Fumba, Zanzibar.
Mkurugenzi wa Huduma za Mamlaka Teophory Mbilinyi  akisaini kitabu mara baada ya kupata maelezo kweye banda la Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) kwenye Maonesho ya Maadhimisho ya miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar yanayofanyika katika viwanja vya Fumba, Zanzibar
Mkurugenzi wa Huduma za Mamlaka Teophory Mbilinyi akipokea zawadi kutoka kwa Mfanyakazi wa TASAC mara baada ya kupata maelezo kweye banda la Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) kwenye Maonesho ya Maadhimisho ya miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar yanayofanyika katika viwanja vya Fumba, Zanzibar

Mkurugenzi wa Huduma za Mamlaka Teophory Mbilinyi akizungumza na Wafanyakazi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) alipotembelea Banda hilo kwenye Maonesho ya Maadhimisho ya miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar yanayofanyika katika viwanja vya Fumba, Zanzibar
Mkurugenzi wa Huduma za Mamlaka Teophory Mbilinyi  akisaini kitabu mara baada ya kupata maelezo kweye banda la Shirika la Reli Tanzania (TRC) kwenye Maonesho ya Maadhimisho ya miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar yanayofanyika katika viwanja vya Fumba, Zanzibar. Kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Habari na Uhusiano TRC Jamila Mbarouk, 
Mkurugenzi wa Huduma za Mamlaka Teophory Mbilinyi  akipata maelezo kutoka kwa  Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano, Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) Salum Pazzy kuhusu kazi zinazofanywa na na Mamlaka hiyo alopotembelea Banda hilo  kwenye Maonesho ya Maadhimisho ya miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar yanayofanyika katika viwanja vya Fumba, Zanzibar. 
Mkurugenzi wa Huduma za Mamlaka Teophory Mbilinyi akizungumza jambo katika Banda la Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) kwenye Maonesho ya Maadhimisho ya miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar yanayofanyika katika viwanja vya Fumba, Zanzibar. 
Picha ya pamoja

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...