KATIBU wa NEC Idara ya Organaizesheni na Mlezi wa Mkoa wa Geita Issa Gavu leo Januari 31, 2024 amekuwa mgeni rasmi katika kuadhimisha Sherehe za Miaka 47 ya CCM kwa kuzindua fremu 107 Kati ya 319 na kushiriki Ujenzi wa frem 80 kati ya 212 na vizimba 700 zinazoendelea kujengwa zilizopo katika wilaya ya Geita Mjini kata ya Katoro Mkoa wa Geita.

Mbali na kuzindua fremu hizo na kushiriki ujenzi wa vizimba pia Issa Gavu amepokea wanachama wapya zaidi ya 4,000 na kukabidhi kadi za Kielekitroniki zaidi ya 32,000 kwa wanachama wa CCM katika Sherehe za miaka 47 ya Chama hicho.

Pamoja na mambo mengine ya Kushekherekea Miaka 47 ya Chama Cha Mapinduzi Mlezi wa Mkoa wa Geita Ndg. Issa Gavu ameongoza tukio la kukata keki mbele ya wanachama wa CCM wilaya ya Geita Mjini na kuwalisha wanachama na viongozi wa Chama pamoja na wananchi waliohudhuria Sherehe hizo katika kata ya Katoro.

Sherehe hizo pia zimeambatana na shamrashara sambamba na kufunguliwa kwa Ofisi ya CCM tawi la Katoro na kuzindua Shina la wakereketwa katika soko la Katoro Senta na kupandisha Bendera ya CCM katika Shina hilo.

Akizungumza wakati akihutubia wananchi na wanachama wa CCM wilaya Geita Mjini katika Kata ya Katoro amewakumbusha kusherehekea miaka 47 ya CCM kwa furaha, amani na utulivu huku akieleza mkatika miaka 47 ya CCM imefanikisha kuleta maendeleo makubwa katika Mkoa wa Geita na wilaya hiyo ya Geita Mjini.

“Tuna kila sababu ya kuendelea kuwa Bora zaidi, tuendelee kukiamini Chama chetu ili tutekeleza Ilani ya CCM kwa vitendo kama ilivyo sasa, "amesema na kuwapongeza Mkoa wa Geita kwa uwekezaji wa vitega Uchumi vya Chama Cha Mapinduzi katika kata na matawi.

“Maduka haya 319 na vizimba 700 tuvitunze na tuimarishe
Mazingira mazuri ya kibiashara ili kuwavutia wawekezaji kuwekeza katika maeneo mbalimbali ya Chama na Serikali”

“Kipindi hichi tunaelekea kwenye uchaguzi naomba tuhimize wanachama na wananchi kwenda kujiandikisha katika daftari la kupiga kura pindi muda utakapofika kusudi tuwe na idadi nzuri na yakuridhisha kushinda kwa Kishindo katika Chaguzi za Serikali za Mitaa na Vijiji."








 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...