BONDIA wa Ngumi za Kulipwa nchini Hassan Mwakinyo aomba Kamisheni ya ngumi visiwani Zanzibar kuweka picha ya Rais wa Zanzibar na Dkt.Hussein Mwinyi kwenye Mikanda ya Mabondia  kutokana na kurudisha mchezo wa ngumi visiwani humo 2023.

Akizungumza Wakati akitambulisha Pambano lake "Mtata mtatuzi" lililoandaliwa na Peaktime Media linalotarajiwa kufanyika Januari 27,2024 visiwani Zanzibar Hassan Mwakinyo dhidi ya bondia Enock Msambudzi kutoka Zimbambwe amesema kitendo cha Rais Dkt. Mwinyi kukubali mchezo wa ngumi kurudi tena visiwani humo ni kitendo cha kishujaa na Ungwana  ambacho viongozi wengi hapo nyuma  walishindwa.

"Kwa kuliheshimu hilo kutoka kwa Rais wetu Dkt.Hussein Mwinyi ningependa kuona Kamisheni ya ngumi upande wa Zanzibar inaweka picha za Rais Mwinyi kwenye mikanda itakayokuwa ikishindaniwa kwenye mapambano yote ili hata vizazi vijavyo vishuhudie uongozi wa Rais huyu ulifanya mapinduzi makubwa katika mchezo wa ngumi

 Mwakinyo amesema kupata nafasi hiyo kucheza pambano hilo ni faraja na ndoto kubwa kuona pambano lake likichezwa visiwani humo na kuleta hamasa kwa damu changa kuongeza uthubutu na kujiamini zaidi kwani wapo  wanaomtazama kama mtu mwenye ushawishi kwao (Role model) kwa mabondia chipukizi.

''Nipo katika maandalizi mazuri sana. Nimejihakikishia hakuna atakayejuta kunishabikia"

Hata Mwakinyo ametumia nafasi hiyo kuomba radhi kwa Mashabiki zake kwa kitendo kilichotokea mwaka 2023 cha kugomea kucheza  pambano lake ilotorajiwa kufanyika Ubungo plaza Jijini Dar es Salaam  2023 na kuleta mtafaruku na  wamajibizano mitandaoni dhidi ya Waandaaji wa pambano hilo Paff promotion.

Kwa upande wake  Muandaaji wa Mapambano kutoka Peaktime Meja Seleman Semunyu amesema wamejiandaa vizuri kutoa burudani visiwani Zanzibar huku akieleza zaidi kuwa mapambano yatakayopigwa Zanzibar ni mjumuisho wa mabondia kutoka mikoa mbalimbali ikiwemo Mbeya,Tanga ,Dar na Zanzibar yenyewe ikiwa mwenyeji mkuu.

Pia ameongeza kuwa kutakuwa na mapambano 11 yatakayopiganiwa katika Uwanja wa Amani Complex Visiwani humo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...