Na Albano Midelo,Songea.

Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Laban Thomas amewaagiza wakuu wa
shule za msingi na sekondari kuhakikisha wanainua kiwango cha ufaulu
kwa wanafunzi na kuunasua Mkoa kwenye ufauli usioridhisha ambao
umedumu kwa kipindi cha miaka mitatu.


Kanali Thomas ametoa agizo hilo wakati anazungumza kwenye kikao kazi
na walimu wakuu wa shule za msingi na wakuu wa shule za sekondari
kilichofanyika kwa nyakati tofauti kwenye ukumbi wa sekondari ya Songea.

“Mtambue kuwa sisi viongozi wenu hatupo tayari kuuona Mkoa unaendelea
kufanya vibaya katika sekta ya elimu,hivyo tumieni kikao hiki kuwa chachu
ya kufanya mabadiliko,mwaka huu tuanze kwa kufanya mabadiliko
makubwa katika utendaji wetu wa kazi ’’,alisisitiza RC Thomas.

Ametahadharisha baada ya kikao hicho hatasikiliza kisingizio chochote kwa
matokeo yasiyoridhisha kwenye mitihani ya kitaifa ambapo amewaagiza
wakuu hao kujirekebisha na kufanya tathmini ya utendaji kazi ili kuongeza
uwajibikaji.

Ili kuhakikisha ufaulu katika elimu ya msingi na sekondari unaongezeka
Mkuu wa Mkoa amewaagiza wakuu wa shule kusimamia na kuinua
taaluma katika shule zao.

Mkuu wa Mkoa pia ameagiza miradi ya ujenzi kusimamiwa ipasavyo na
kusimamia fedha za serikali zinazotolewa kwa uendeshaji wa shule.

Maagizo mengine ambayo ameyatoa ni kila shule kupanda miti ya
matunda,kushirikiana na jamii katika kuleta maendeleo ya shule,kuboresha
mazingira ya shule,kujiepusha na mikopo inayotolewa na Taasisi zisizo za
kibenki na kutekeleza agizo la kila shule kulima hekari tano za mazao ya
nafaka,mbogamboga na matunda.

Awali akitoa taarifa ya elimu ya msingi na sekondari kwenye kikao
hicho,Afisa Elimu wa Mkoa wa Ruvuma Mwl,Edith Mpinzile amesema
Mkoa umeendelea kufanya vibaya kwenye matokeo ya mtihani wa kitaifa
kwa kuwa Mkoa umeshindwa kufikia lengo la ufaulu lililowekwa kitaifa la
asilimia 85 kwa mitihani ya kuhitimu elimu ya msingi na asilimia 100 ya
upimaji wa mitihani ya darasa la nne.

Ameutaja ufaulu wa darasa la saba mwaka 2023 ulikuwa ni asilimia 69.9
na ufaulu wa darasa la nne ni asilimia 76.01 ambapo amesema Mkoa pia
umeendelea kufanya vibaya katika mitihani ya sekondari ya kitaifa kwa
kuwa Mkoa umeshindwa kufikia lengo la ufaulu la asilimia 100 kwa mtihani
wa upimaji wa kidato cha pili ambapo ufaulu wa Mkoa mwaka 2023 ulikuwa
ni asilimia 81.96.

Hata hivyo amesema Idara ya Elimu Ofisi ya Mkuu wa Mkoa imebaini
mambo mbalimbali yanayosababisha ufaulu usioridhisha ambayo
ameyataja kuwa ni baadhi ya walimu wanashindwa kutekeleza majukumu
yao ya kila siku,mada hazikamilishwi na walimu hawatoi mazoezi na
majaribio ya kutosha.

Changamoto nyingine amezitaja kuwa ni baadhi ya walimu hawazungumzi
na wanafunzi kujua changamoto zao,walimu hawakai kwenye vituo vya
kazi,walimu hawana ubunifu na walimu kuwa na madeni yaliyopitiliza
ambayo yanaondoa utulivu kazini hivyo walimu wanashindwa kufundisha
kikamilifu.

Mkoa wa Ruvuma una shule za msingi 841 na shule za sekondari 233


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...