*Rehema atoa rai wanawake kuachana na kusemana

Na Chalila Kibuda,Michuzi TV

Naibu Spika Mussa Azzan Zungu amesema kuwa wanawake wajitoe kumuunga mkono Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa jitihada zake katika kuwakomboa kiuchumi.

Zungu ameyasema hayo wakati wa uzinduzi wa Jukwaa la Uwezeshaji Wanawake Kiuchumi Kata ya Kivukoni ,amesema kuwa wakiweka dhamira ya kujikomboa kiuchumi watafika mbali kwani Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan yuko nyuma yao kwa kuweka mazingira ya kufanya uwezeshaji wa wanawake utimie.

Amesema kuwa mikopo kwa kata ya Kivukoni kwa miaka mitatu iliyopita ilikuwa milioni 800 kwa sasa itakwenda mara ya tatu ya hizo fedha za zilizokuwa zimetolewa .

Aidha amesema mikopo itakayotolewa katika vikundi ziende katika biashara na sio kuzielekeza kwenye sherehe za kuzaliwa ambazo sio dhamira yake.

Naibu Spika ametaka kikindi hicho kijisajili na ndipo kuwasaidia na yeye pamoja na kuwa mlezi wa jukwaa hilo.

Mwenyekiti wa Jukwaa la Uwezeshaji Wanawake Kiuchumi Wilaya ya Ilala Rehema Sanga amesema wanawake umefika wakati kwa kushikana mkono Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan katika kuweza Rais huyo kutimiza matarajio ya wanawake.

Rehema amesema kuwa majukwa ya wanawake kila kila kata ya Manispaa ya Ilala yameanzishwa na shughuli za kuendesha za kiuchumi zinafanyika.

Amesema silaha kubwa ya wanawake kujikwamua kiuchumi ni kuachana na kusemana kwa mambo ya sio kuwa ya msingi.

Rehema amesema sasa wakati ni wetu wa kuonyesha tunaweza kuwa tofauti kutokana na kuwa na kiongozi wetu pale juu Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan.

Hata hivyo amesema kuwa majukwaa yote kuwa na uchungu na fedha wanazokopeshwa kwa kurudisha ili wengine nao waweze kukopa.
 

Naibu Spika Mussa Azzan Zungu akizungumza wakati wa Uzinduzi wa Jukwaa la Uwezeshaji Wanawake Kiuchumi Kata ya Kivukoni jijini Dar es Salaam.
 

Mwenyekiti wa Jukwaa la Uwezeshaji Wanawake Kiuchumi Rehema Sanga akitoa maelezo kuhusu majukwaa yanavyofanya kazi katika kuwawezesha wanawake kiuchumi.
 

Mwenyekiti wa Jukwaa la Uwezeshaji Wanawake Kiuchumi Rehema Sanga akizungumza na waandishi wa habari   kuhusu majukwaa yanavyofanya kazi katika kuwawezesha wanawake kiuchumi.

 

Matukio katika picha ya Keki mara baada ya uzinduzi wa Jukwaa la Uwezeshaji  Wanawake Kiuchumi Kata ya Kivukoni.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...