Naibu Waziri wa Uchukuzi David Kihenzile, Katibu Mkuu Wizara ya Uchukuzi Prof. Godius Kahyarara pamoja Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi Dkt. Ali Possi wametembea banda la Kampuni ya Huduma za Meli (MSCL) lilipo katika Maonesho ya Biashara ya Kimataifa Zanzibar.
Naibu waziri Kihezile mara baada ya kutembelea Banda hilo alisisitiza kuendelea kuitangaza meli ya mizigo ya MV. Umoja inayofanya safari zake kati ya Mwanza, Tanzania na Portbell na Jinja, Uganda pamoja na Kisumu nchini Kenya.
Pia naye Katibu Mkuu Wizara ya Uchukuzi Prof. Godius Kahyarara ameipongeza Kampuni ya Huduma za Meli (MSCL) kwa kushiriki katika Maonesho hayo kwani ni fursa nzuri ya kuwasiliana, kujifunza na kubadilishana taarifa na maarifa na wadau wa sekta ya usafirishaji.
Katibu Mkuu Wizara ya Uchukuzi Prof. Godius Kahyarara akisaini kitabu kwenye banda la Kampuni ya Huduma za Meli (MSCL) alipotembelea banda hilo akiambatana na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi Dkt. Ali Possi kwenye Maonesho ya Maadhimisho ya miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar yanayofanyika katika viwanja vya Fumba, Zanzibar.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...