Na Janeth Raphael MichuziTv- Dodoma.


Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mh. Nape Nnauye ameitaka Bodi ya Tume ya PDPC kutekeleza majukumu yake kwa kuzingatia Sheria, kanuni na miongozo iliyowekwa na si kwa Matakwa na Utashi wa watu fulani.

Waziri Nape ameyasema hayo leo hii Jijini Dodoma katika Uzinduzi wa Bodi ya Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi (PDPC)

Na kuongeza kuwa anatamani kuona time hii Inakuwa huru na kutoingiliwa kwa namna yeyote kwani Sheri na miongozo ipo wazi.

"Natamani tume muhakikishe, tume inaanza kutekeleza majukumu yake kwa kuzingatia Sheria,kanuni na miongozo mbalimbali iliyowekwa. Kama kuna tume tunataka iwe huru kutekeleza majukumu yake hii tume nataka iwe huru mlinde hilo,tusiingilie na nyie msikubali kuingiliwa mlindwe na Sheria tumezitunga,ziko kanuni kama kuna shida mahali ni Bora turekebishe Sheria na kanuni,lakini msiendeshwe kwa Matakwa na Utashi wa watu tuendeshe kwa mujibu wa sheria".

Aidha Waziri Nape amewataka viongozi wa Bodi ya Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi kuilinda Imani ya Raisi juu yao kwa kuwekwa katika nafasi kwa kutekeleza majukumu yao kwa tija,ufanisi na uzalendo na asitokee mtu yeyote kuupuuza Imani hiyo

"Mmepewa Kazi ya kutujengea msingi ambao wengi watakapokuja watajenga katika msingi ambao mmeujenga nyie,kwahiyo jukumu lenu ni kubwa Raisi amekuwa na Imani na nyie na sisi tuna Imani na nyie pia, kwahiyo Raisi kuwa na Imani na nyie maana yake kwa niaba ya Watanzania Raisi amewaamini, hii Imani kubwa ambayo kama viongozi wa tume mnapaswa kulinda na kusimamia majikumu ya Tume kwa tija, ufanisi na uzalendo kama nilivyosema Raisi amefanya kwa niaba ya Watanzania kuwaamini nyie, hivyo asitokee mtu akaipuuza Imani hii"

Pia amaelezea namna Tume hii ilivyo kuwa na nafasi kubwa ya kulinda Heshima,Haki na Utu wa mtu kwa taarifa zao zinavyotumika katika njia inayozingatia Haki.

"Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi Ina jukumu kubwa la kulinda Heshima, Haki na Utu wa watu kwa kuhakikisha taarifa zao binafsi zinatumika kwa njia inayozingatia Haki, Heshima na Utu wao,tunataka taarifa za watu katika Nchi yetu, Watanzania,Wageni na wote watakaokuja katika Nchi hii wawe na hakika kuwa taarifa zinatumika katika njia inayozingatia Haki Heshima na Utu wa mtu,Tunatamani Nchi hii Iheshimike Duniani kwa kuheshimu Haki ya taarifa za watu, Heshima ya taarifa za watu ili watu wakimbilie Taifa letu na kuona ni sehemu sahihi".

Pia Waziri amesema si vibaya kwa Bodi kujifunza kwa Nchi ambazo zilianza na mfumo huu ili kuona wapi zilipofanikiwa na penye mapungufu tuone namna ya kufanya maboresho.

" Wapo waliotangulia hivyo mnaweza kujifunza kutoka kwao wamefanyaje vizuri,wamekosea wapi sisi tuone namna tunavyoweza kuboresha. Ni matumaini yangu baada ya muda mfupi watu waje Tanzania kujifunza namna Bora ya kulinda Utu na Heshima za watu"

Naye Katibu Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mohammed Khamis Abdulla ametumia nafasi hii kutoa Rai kwa Bodi hii kuhakikisha wanatekeleza majuku ya msingi kama yalivyoainishwa katika Sheria na kanuni zake.

"Mheshimiwa Waziri kwa kuwa kikao hiki mahsusi kwako kwa kutoa maelekezo,nitumie nafasi hii kutoa Rai kwa Bodi kuhakikisha wanatekeleza majukumu ya msingi kama yalivyoainishwa kwenye sheria,kanuni na miongozo uliotolewa na Msajili wa Hazina pamoja na ahadi zako ulizotoa kwenye Hotuba ya Bunge ya mwaka 2023/2024".

Awali akitoa taarifa fupi ya PDPC,Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi hii ACP Emmanuel Mkilia amesema Bodi imepata matokeo kwa asilimia 90 ndani ya siku 100 kwa Mambo iliyokuwa imejiwekea ikiwemo kujenga uwezo wa Taasisi na pia kujenga uwezo kwa Watumishi wao.

"Matokea yetu ambayo tumeyafanya katika hizi siku 100 tulifanikiwa kwa kiwango cha asilimia 90 kwa Mambo Yale ambayo tulijipangia kufanya huku tukiwa tunajipima,kujenga uwezo wa Taasisi na kujenga uwezo wa Staff pia".

Tume ilianza kutekeleza majukumu yake Rasmi tarehe 1 May 2023 ikiwa ni utekelezaji wa Sheria ya Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi namba 11 ya mwaka 2022.
 

Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Nape Nnauye (Mb) akizungumza wakati wa Uzinduzi wa Bodi ya Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi uliofanyika katika ukumbi wa TCRA, jijini Dodoma leo Januari 19, 2024.
 

Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Nape Nnauye (Mb) akizindua Bodi ya Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi katika ukumbi wa TCRA, jijini Dodoma leo Januari 19, 2024. Kulia ni Mwenyekiti wa Bodi hiyo, Balozi Adadi Mohammed na kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Bw. Mohammed Khamis Abdulla.
 

Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Nape Nnauye (Mb) akizindua Bodi ya Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi katika ukumbi wa TCRA, jijini Dodoma leo Januari 19, 2024. Kulia ni Mwenyekiti wa Bodi hiyo, Balozi Adadi Mohammed na kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Bw. Mohammed Khamis Abdulla.
 

Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Nape Nnauye (Mb) pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo wakiwa katika picha ya pamoja na Bodi ya Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi katika ukumbi wa TCRA, jijini Dodoma leo Januari 19, 2024.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...