Mwenyekiti Taifa wa Chama cha NCCR – MAGEUZI Haji Ambar Khamis amempongeza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dk. Hussein Ali Mwinyi kwa kusimamia vyema maadhimisho ya miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa Amani na umoja.

Ameyasema hayo huko katika Ukumbi wa Sanaa, Rahaleo wakati akizungumza na waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali

Amesema, miradi iliyozinduliwa na Serikali ya Dr. Mwinyi katika maadhimisho hayo imedhihirisha kazi kubwa aliyoifanya ya kuwatumikia Wananchi hivyo chama hicho kitaendelea kushirikiana naye ili kuleta maendeleo Nchini.

Hata hivyo amesema chama hicho hakitashiriki Maandamano ya Amani yaliyotangazwa na Chama cha Demikrasia na Maendeleo (CHADEMA) kufanyika Nchini ya kupinga marekebisho ya sheria ya Uchaguzi kwa vile chama hicho kimeshapeleka mapendekezo yao katika marekebisho hayo.

Amesema maandamano si njia sahihi ya kutafuta muafaka wakati zipo njia mbadala za kutafuta suluhu pale mnapotofautiana hivyo amewataka wanachama wa chama hicho kutokujihusisha na Maandamano hayo.



Mwenyekiti wa chama cha NCCR Mageuzi Taifa Haji Ambar Khamis akizungumza na waandishi wa habari wakati akitoa pongezi kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Hussein Ali Mwinyi kwa kuadhimisha miaka 60 ya Mapinduzi katika hali ya amani na upendo ,Hafla iliyofanyika Ukumbi wa studio rahaleo Mjini Unguja.

PICHA NA FAUZIA MUSSA-MAELEZO ZANZIBAR

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...