Kampuni ya kimataifa ya Old Mutual Limited leo imetangaza kuuza hisa zake zote za biashara yake ya muda mfupi ya bima kwenye kampuni ya bima ya UAP Insurance Tanzania, kwa kikundi cha wanahisa wenye hisa chache ndani ya kampuni ya UAP Insurance. 

Mauzo ya hisa hizo yatakuwa rasmi baada ya kuidhinishwa ya mamlaka za udhibiti wa bima nchini.

Uamuzi huu unafuatia mapitio ya kina ya kimkakati ya biashara kwa kuzingatia malengo ya muda mfupi na ya muda mrefu ya kampuni ya Old Mutual.

Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Old Mutual Holdings, Arthur Oginga alisema: “Tangu tuinunue UAP Insurance Tanzania mwaka 2015, imekuwa ni dhamira yetu kukuza biashara kwa lengo la kuifanya kampuni hiyo iwe miongoni mwa watoa huduma za kifedha wanaoongoza kwenye soko la huduma hizo nchini Tanzania. 

Katika kutekeleza hilo tulifanya uwekezaji wa kimkakati ili kuhakikisha kuwa biashara yetu inabaki kwenye msingi imara na kuweza kushindana kwa mafanikio.

 Hata hivyo, biashara nchini Tanzania imekabiliwa na changamoto katika kurudisha mtaji kutokana na sababu mbalimbali za kiutendaji na kimazingira.

 Tumetathmini mikakati mbalimbali ya kupata uongozi wa soko nchini Tanzania lakini hatuoni tena njia ya kufikia lengo hili la kimkakati. 

Tathmini yetu imeonyesha kwamba tutahitaji kufanya uwekezaji mkubwa zaidi ili kufikia malengo ya uongozi wa soko.

 Kutokana na hali hiyo, tumeamua kuuza hisa zetu kwa Strategic Ventures Company Limited, muungano kutoka kwa wanahisa wachache wa UAP Insurance Tanzania Limited.

”UAP Insurance Tanzania imesema huduma na mahusiano na wateja na wadau wake nchini Tanzania vitabaki vilevile na itashirikiana na wamiliki wanaoingia ili kuendeleza huduma thabiti kwa wateja.

 "Tunatumia fursa hii kuwataarifu wateja wetu na wadau wetu kwamba watarajie kuendelea kupata huduma bora zaidi."Uwekezaji wa Old Mutual kwenye ukanda wa Afrika Mashariki bado ni thabiti. Hata hivyo, ukuaji huu unahitaji kuwa endelevu, kwa maslahi mapana ya wadau.”"

Katika kipindi cha miaka miwili iliyopita, tuliamua kutumia jina la Old Mutual ili kuimarisha chapa yetu hapa Afrika Mashariki.

Katika mwaka ujao, zoezi hili litaendelea, na tutaimarisha uwekezaji wetu ili kukuza biashara na kuendelea kuwa bora katika huduma jumuishi za kifedha," aliongeza Oginga.Oginga alihitimisha:

 “Tunawashukuru watu wa Tanzania kwa kutumia huduma za UAP Insurance na kampuni ya Old Mutual. Tunajivunia sana biashara ambayo tumeweza kuijenga nchini na kwa ufanisi wa timu yetu.”



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...