Na Raisa Said,Tanga


UTEKELEZAJI wa Programu Jumuishi ya Taifa ya Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto ( PJT-MMMAM)unaweza kutoa suluhisho la kudumu la chanagamoto inayokabili wilaya ya Pangani ya ukatili wa kijinsia dhidi ya watoto hususan walio kati ya umri wa miaka 0 hadi nane.

Hayo yemeelezwa leo na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Pangani,Veronica Marwa, akizungumza katika mahojiano mara baada ya uzinduzi Wa programu hiyo ngazi ya Halmashauri.

Amesema kitakwimu Wilaya ya Pangani inaonekana ina changamoto kubwa ya ukatili wa kijinsia dhidi ya watoto wenye umri kuanzia Mwaka 0-8 lakini hilo linawezekana kutokana na ukosefu wa malezi, makuzi na maendeleo ya awali ya watoto.

“Pengine mtoto anakua katika mazingira ambayo anakuwa anasikia watu wanatukana, wanafanya hiv..., pengine anaona kuwa ni mambo ya kawaida. Utekelezaji wa Programu hii utasadia kuondoa tatizo hilo la ukatili wa kijinsia, kwa watoto wenye umri kuanzia miaka o -8 ” alisisitiza Marwa.

Marwa ambaye ni Ofisa Utumishi wa Halmashauri hiyo ya Pangani alieleza kuwa Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Pangani imeandaa programu ambayo inayohusu ukatili wa Kijinsia akaahidi kushirikiana kuona namna gani ya kuzuia au kuondoa kabisa ukatili wa kijinsia kwa watoto waliopo katika wilaya hiyo,

Pia amewataka viongozi wote kuhakikisha wanaingiza masuala ya malezi na makuzi ya watoto katika bajeti zao ukichukulia kuwa hivi sasa ni wakati wa kuandaa bajeti.

“Tunaona kuwa program inahitaji fedha nyingi kwa ajili ya utekelezaji wake lakini hakuna mahali inaonyesha kuwa kuna mdau ataleta fedha kwa ajili ya utekelezaji ya programu. Tunatakiwa kutumia raslimali zilizopo katika uetekelezaji,” amesema.

Amemwagiza Ofisa Ustawi wa Jamii wa halmashauri hiyo kwenda kuchambua zile shughuli za muda mfupi ambazo wanaweza kuanza nazo katika sekta mtambuka.

Ametoa kwa mfano katika miradi ya Tasaf inawezekana kuisaidia jamii kuibua miradi itakayosaidia utekelezaji wa program hii.

Kwa mujibu wa Ofisa Ustawi wa Wilaya hiyo Kirigiti Matera amesema ukatili dhidi ya watoto walio chini ya umri wa miaka 0-8 unafika asilimia 86 nakwamba mwezi uliopita kuna kesi tano ambazo zimefikishwa katika mahakamani ambapo Kesi hizo zinahusu ukatili dhidi ya watoto. Alitaja vitendo vya uakatili ni pamojana kubakwa na ulawiti.

“Mwezi uliopita kulikuwa na kesi tano ambazo zimefikishwa mahakamani zinahsu ukatili dhidi ya watoto. Hata jana tu nilikuwa mahakamani kwenye kesi ya ukatili dhidi ya mtoto mmoja,” amesema Kirigiti.

Wakati huo huo Kaimu Mkurugenzi wa Jiji,akizungumza baada ya uzinduzi wa Programu hiyo jijini Tanga amesisitiza kuhusu umuhimu wa mpango huo, ambapo amesema hivi sasa kuna tatizo kubwa la mmomonyoko wa maadili katika jamii.

Amesisitiza juu ya haja ya kujifunza ili kuwapa watoto malezi na makuzi sahihi huku akifafanua majeraha waanayopata watoto wenye umri mdogo ya ukatili yanadumu kwa muda mrefu mno katika maisha yao.

“Kama Serikali imekuja na mpango lazima tuukubali kutokana na mambo tunayoona yanayoendelea katika jamii. Kama tusipochukua hatua sahihi hivi sasa basi tutegemee kuwa na kizazi kibovu sana hapo baadaye,” amesema.

Awali Mkurugenzi wa Shirika la United Help for Tanzania Children (UHTC), Dk. Regis Temba amesema kuwa hivi sasa baada ya uzinduzi wa kimkoa wanafanya uzinduzi katika ngazi ya Halmashauri.

"Mpaka sasa tumeshafanya uzinduzi katika halmashauri tatu ambazo ni Mkinga, Tanga Jiji na Pangani. Shirika hili ndilo shirika mwenyeji wa Programu hiyo mkoani Tanga."

Ameongez bado elimu inahitajika kufika katika ngazi za kata na vijiji, sehemu ambazo alisema ndiko kwenye watu wengi. Pia alizungumzia juu ya haja ya kutoa elimu katika kliniki za uzaz ili kina mama wawe na uelewa wa kutosha.

Dk.Temba amesema wataendelea kutoa elimu kwa jamii kupitia vyombo vya habari kama vile redio, magazeti ,mitandao ya kijamki na televisheni ili kusaidia jamii kulea watoto kwa mujibu wa nguzo tano za malezi ya watoto.

Kwa upande wake Ofisa Ustawi wa Jamii Mkoa wa Tanga Mmasa Mulugu ambaye ni Mratibu wa Programu hiyo ameahidi kujenga timu imara ambayo itasaidia katika utekelezaji wa Programu hiyo kwa ufanisi zaidi kaika mkoa.





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...