Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiwa na Waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda Zanzibar Mhe. Omar Said Shaabani pamoja na viongozi mbalimbali wakati akikata utepe kuashiria ufunguzi wa Jengo la Kitega Uchumi la Shirika la Biashara la Taifa Zanzibar (ZSTC) lililopo Chakechake Pemba tarehe 09 Januari, 2024.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na viongozi mbalimbali mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Ndege wa Pemba kwa ajili ya ziara ya kikazi tarehe 09 Januari, 2024.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiangalia kikundi cha ngoma ya Kibati ikitumbuiza mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Ndege wa Pemba kwa ajili ya ziara ya kikazi tarehe 09 Januari, 2024.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimsikiliza Mkurugenzi Mwendeshaji wa Shirika la Taifa la Biashara Zanzibar (ZSTC) Soud Said Ally kuhusu Kituo cha kupimia Karafuu kilichopo katika jengo hilo la Kitega Uchumi la ZSTC Pemba tarehe 09 Januari, 2024.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akivuta kitambaa pamoja na Waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda Zanzibar Mhe. Omar Said Shaabani kuashiria ufunguzi wa Jengo la Kitega Uchumi la Shirika la Biashara la Taifa Zanzibar (ZSTC) lililopo Chakechake Pemba tarehe 09 Januari, 2024.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...