Na Pamela Mollel,Simanjiro .
Mkuu wa Mkoa wa Manyara Queen Sendiga amewataka wananchi kutii sheria bila shuruti huku akitoa wito kwa wahifadhi kuendelea kutoa elimu kwa jamii inayozunguka maeneo ya hifadhi ili na wao waweze kujua uhifadhi na kuepuka migogoro baina ya hifadhi na wananchi
Alitoa rai hiyo januari 16,2024 katika kijiji cha Kimotorok wilaya ya Simanjiro mkoani Manyara wakati akizungumza na Viongozipamoja na wananchi wa eneo hilo,akitatua mgogoro uliodumu kwa muda mrefu baina ya hifadhi ya Tarangire na wananchi wa kijiji cha Kimotorok
Alisema kuwa wananchi wanapaswa kutii sheria zilizopo kwa kuwa eneo hilo ni la hifadhi ya Tarangire na tayari lina mipaka yake ya kudumu hivyo eneo hilo haliruhusiwi kufanya shughuli zozote isipokuwa za uhifadhi
Kwa upande wake Kamishna Msaidizi Mwandamizi,Beatrice Kessy anasema wao kama hifadhi wataendelea kutoa elimu kwa wananchi kuhusu uhifadhi pamoja na kuendeleza shughuli za ujirani mwema
"Kumalizika kwa mgogoro huu unafungua fursa za utalii ukanda wa kusini mwa Tarangire ambapo wananchi waliopo katika kijiji hicho watanufaika na utalii huo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...