Shule ya Sekondari ya Royal Family iliyoko Kata ya Buhalahala katika Halmashauri ya Mji wa Geita ambayo imefanya vizuri katika matokeo ya kidato cha nne hali iliyopelekea wazazi wa watoto shuleni hapo kufurahushwa na kurudhishwa na matokeo ya kidato cha pili ya shule hiyo yaliyo tangazwa na Baraza la Mihani la Taifa (Necta) Januari 7 mwaka huu.


Akizungumza na vyombo vya habari shuleni hapo mmoja wa wazazi, Bestina Malila amesema kuwa matokeo hayoyamemridhisha,kumfurahisha na yamempa imani kuwa mtoto wake yuko shule sahihi na yuko kwenye mikono salama kitaaluma .

Aidha ameeleza kuwa amepata imani kuwa mtoto wake ambaye anasoma kidato cha nne atafanya vizuri katika mtihani wa Taifa kwani matokeo hayo yanaonyesha shule hiyo ina walimu wenye uwezo mkubwa wa kuandaa wanafunzi katika masoma yao.

Mkuu wa shule hiyo Elikana Simon amesema kuwa malengo ya shule hiyo ni kuakikisha wanafunzi wote wnapata daraja la kwanza kwasababu wana walimu wa kutosha, mazingira ya kufundishia kama vile madarasa ,maabara na maktaba ya kisasa yanayosaidia mwanafunzi kujifunza kikamilifu.

Mwalimu Simon amesema kuwa Uongozi wa shule hiyo unahakikisha walimu wanalipwa kwa wakati nmotisha mbalimbali pamoja wanafunzi kupata haki zao kwa usahihi kama vile chakula bora na vifaa vya kujifunzia ili waweze kusoma kwa bidii.

Naye mwalimu wa taaluma wa Royal Family Dickson Range anasema kuwa moja ya vichocheo vinavyo sababisha shule hiyo kufanya vizuri kitaaluma katika matokeo ya taifa ni motisha ambayo Mkurugenzi wa shule hiyo aliitoa kwa walimu kufundisha masomo ya ziada na kuwalipa waliofundisha masomo ya ziada.

Amesema kuwa muda wa ziada ukifika baada ya muda wa masomo, walimu wote wanaofundisha vipindi hivyo vya ziada Mkurugenzi analipia vipindi hivyo ambayo ni malipo ya ziada tofauti na Mishahara yao ya kila mwezi ,jambo ambalo linawatia chachu walimu kufundisha kwa moyo na kwa kujituma.

Aidha amesema kuwa shule hiyo imejidhatiti katika maabara za sayansi ambazo ni maabara ya kemia ,fizikia na Biolojia ambazo zina vifaa vya kuwawezesha kusoma kwa vitendo masomo ya sayansi na kuwawezesha kufaulu mitihani yao ya taifa.

Akizungumzia matokeo ya kidato cha pili ya shule hiyo,mwalimu huyo wa taaluma amesema kuwa wanafunzi wapatao 25 wamepata daraja la kwanza la pointi za digiti moja (single digit) ambazo ni pointi 7 na 8 ,wanafunzi 7 walipata pointi daraja la kwanza pointi 13 na wanafunzi 2 ndiyo waliopata darajala pili pointi 18 na pointi 20.

Katika matokeo hayo shule ya Royal family Sekondari kati ya wanafunzi 34, Necta ilitangaza kuwa wanafunzi wapatao 32 walipata daraja la kwanza (Division one) na wanafunzi wawili tu ndiyo waliopata daraja la pili (division two).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...