Kampuni ya Samsung imezindua simu janja (Smartphones) tano mpya za Galaxy ambazo ni mwendelezo wa simu bora za kampuni hiyo zinazotawala katika masoko nchini kutokana na kupendwa na watumiaji wake wengi. Simu mpya zilizozinduliwa ni aina ya Galaxy A25 5G, Galaxy A15 5G, Galaxy A15, Galaxy A05s na Galaxy A05, zimetengezenezwa kwa vionjo mbalimbali kukidhi matakwa ya wateja wa bidhaa za Samsung wapya na wateja wa siku zote na zinapatikana kwa bei nafuu.

Galaxy A25 5G, inawezesha matumizi bora ya simu ya mkononi ikiwa na mwonekano maridadi wa inchi 6.5 FHD na rangi angavu yenye mwonekano maridhawa. Mwonekano wa 120Hz pia huhakikisha utumiaji wa haraka, kucheza michezo, kuperuzi, kutazama video na kusoma makala. Simu inayo kamera ya OIS yenye uwezo tofauti ya 50MP ambayo hupiga picha zenye mwonekano mzuri na zinazong'aa bila kuzitikisa kutokana na kuwa na lenzi yenye uwezo mkubwa wa kunasa picha katika mazingira mbalimbali, kwa kuitumia inaleta matokeo mazuri na burudani katika maisha ya kila siku.

Galaxy A15 5G, wateja watakuwa na simu mahiri yenye kasi, ya kutegemewa na maridadi ambayo inaweza kuwasaidia kuweka matukio yote ya kukumbukwa. Kila picha na video inayonaswa kwa kutumia kamera ya juu zaidi ya 50MP ya Galaxy A15 5G, na faili nyingine zote muhimu zitahifadhiwa kwa usalama kwa hisani ya kumbukumbu ya kutosha ya 6GB na hifadhi inayoweza kupanuliwa ya 128GB, kukupa utendakazi mzuri na nafasi ya kutosha kwa maisha yako ya kidijitali.

Galaxy A15 LTE, ina mwonekano wa inchi 6.5 la FHD+ Super AMOLED 90hz, yenye kioo kikubwa chenye rangi angavu zinazohitajika kwa mahitaji ya kila siku katika kurahisisha maisha ya mtumiaji kutokana na mwonekano wake wa kupendeza na kuwa rahisi kuitumia sambamba na gharama yake kuwa nafuu.

Galaxy A05s ni simu maridadi yenye program mbalimbali za kisasa. Wateja wataweza kueleza ubunifu wao na kutengeneza kumbukumbu nzuri kwa kutumia mfumo wa kamera tatu za Galaxy A05s. Mbali na kuwa na ufikiaji wa programu na media zote zinazopendwa zilizopo, watumiaji wanaweza kusalia wameunganishwa siku nzima kwa kutumia betri ya muda mrefu ya Galaxy A05s na kufurahia urahisi wa kuchaji 25W kwa kasi.

Kwa thamani kuu kutoka kwa simu janja utaipata kwa kutumia simu ya Galaxy A05. Watumiaji watafurahia michezo, mfululizo, filamu, video za Tik Tok na reels za Facebook na maudhui mengine yoyote kutoka kwa skrini ya inchi 6.7 ya HD+. Kamera mbili za simu huleta furaha maradufu inapokamata ulimwengu kwa pembe tofauti.

Bei ya simu hizi mpya katika za Galaxy zilizozinduliwa katika soko la Tanzania ni:

• Galaxy A25 5G itagharimu shilingi 905,000 ikiwa na ukubwa wa kuhifadhi kumbukumbu kiasi cha GB8 na hifadhi ya kiwango cha GB 256, na simu yenye ukubwa wa kuhifadhi kumbukumbu ya GB 6 na hifadhi ya GB 128 itagharimu shilingi 775,260.

• Kumbukumbu ya Galaxy A15 5G 6 GB na hifadhi ya GB 128 itagharimu Tzs591,000, na kumbukumbu ya GB 4 na hifadhi ya GB 128 itagharimu Tzs548,000

• Kumbukumbu ya Galaxy A15 LTE ya GB 6 na hifadhi ya GB 128 itagharimu Tzs503,000, na kumbukumbu ya GB 4 na hifadhi ya GB 128 itagharimu Tzs463,000

• Kumbukumbu ya Galaxy A05s ya GB 6 na hifadhi ya GB 128 itagharimu Tzs445,000, kumbukumbu ya GB 4 na hifadhi ya GB 128 itagharimu Tzs404,000 na kumbukumbu ya GB 4 na hifadhi ya GB 64 itagharimu Tzs363,000.

• Hifadhi ya Galaxy A05 GB 4 na kumbukumbu ya GB 128 itagharimu Tzs326,000 na kumbukumbu ya GB 4 na hifadhi ya GB 64 itagharimu Tzs284,000.

Simu zote hizi mpya za Galaxy A zimeanza kupatikana katika maduka yote ya chapa ya Samsung na wauzaji walioidhinishwa kuanzia tarehe 1 Januari 2024. Galaxy A25 5G, A15 5G na A15 zinakuja na Samsung Care+, ambayo hutoa ulinzi wa miezi 12 dhidi ya uharibifu wa skrini kwa bahati mbaya. Wateja wanaohitaji kununua simu wanahimizwa kujiandikisha kwenye Samsung Care+ ndani ya siku 30 za ununuzi na kupata walanti kwa kipindi cha miezi 12.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...