Na Mwandishi Wetu, Dodoma

SERIKALI imesema inaendelea na utekelezaji wa miradi ya kipaumbele ya umeme itokanayo na nishati ya Jotoardhi katika maeneo mbalimbali nchini kupitia Kampuni ya Uendelezaji Jotoardhi Tanzania (TGDC).

Hayo yameelezwa leo Januari 18, 2024 na Naibu Waziri wa Nishati, Judith Kapinga jijini Dodoma wakati wa semina ya kuwajengea uwezo wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini kuhusu Rasilimali ya Jotoardhi

Amesema kwamba miradi ya kuzalisha umeme kutokana na Jotoardhi inayoendelea kutekelezwa nchini ni Ngozi 70MW na Kiejo - Mbaka 60MW iliyopo Mbeya, Sogwe 5MW, Luhoi 5MW mkoani Pwani na Natron 60MW uliopo Arusha.

"Kati ya miradi hiyo mitano, miradi minne ipo katika hatua ya uhakiki wa rasimali ya Jotoardhi na mradi mmoja wa Natron upo katika hatua ya utafiti wa kisayansi wa kina," amesema Naibu Waziri Kapinga.

Amesisitiza kuwa suala la sheria ya Uendelezaji miradi ya Jotoardhi litafanyiwa kazi na Serikali ili kuhakikisha ifikapo mwaka 2025/2026 kuwe na uzalishaji wa Megawati 30 kutokana na umeme wa Jotoardhi.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini Mathayo David Mathayo amepongeza Serikali kwa kuendelea kutekeleza miradi mbalimbali ya umeme inayotokana na Jotoardhi.

Semina hiyo imehudhuriwa na Katibu Mkuu Wizara ya Nishati Mhandisi Felchesmi Mramba, Kamishna wa Umeme na Nishati Jadidifu Mhandisi. Innocent Luoga na watendaji wengine kutoka Wizara ya Nishati, Shirika la umeme Tanzania (TANESCO) na Kampuni ya Uendelezaji ya Jotoardhi Tanzania (TGDC).
Mwenyekiti wa Kamati ya  Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini Mathayo David Mathayo akiongoza semina ya kuwajengea uwezo wajumbe kuhusu Rasilimali ya Jotoardhi iliyofanyika Januari 18, 2024, jijini Dodoma.
Naibu Waziri wa Nishati Judith Kapinga akizungumza jambo wakati wa semina ya kuwajengea uwezo wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini iliyofanyika Januari 18, 2024, jijini Dodoma

Meneja Mkuu wa Kampuni ya Uendelezaji Jotoardhi Tanzania Mhandisi Mathew Mwangomba akitoa elimu ya nishati ya jotoardhi katika semina ya kamati ya kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, Bungeni Dodoma tarehe 18 januari, 2024.

Katibu Mkuu Wizara ya Nishati Mhandisi Felchesmi Mramba akizungumza jambo wakati wa semina ya kuwajengea uwezo wajumbe wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini kuhusu Rasilimali ya Jotoardhi.
Wajumbe wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, wakiwa pamoja na Watendaji Mbalimbali wakati wa semina ya kuwajengea uwezo kuhusu Rasilimali ya Jotoardhi, iliyofanyika jijini Dodoma, Januari 18, 2024.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...