WAF - Dar es Salaam
SERIKALI kupitia Wizara ya Afya imeongeza kasi ya kutoa elimu na dawakinga kwa jamii ili kuyatokomeza magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele ifikapo 2030.

Amesema, mafunzo hayo ni sehemu ya maandalizi kuelekea Maadhimisho ya Siku ya Magonjwa yaliyokuwa Hayapewi Kipaumbele Duniani (matende na mabusha, Usubi, Trakoma, Kichocho na Minyoo ya tumbo) inayotarajiwa kufanyika Januari 30, mwaka huu.
“Mwaka huu tumejipanga kuadhimisha Siku ya Magonjwa yaliyokuwa Hayapewi Kipaumbele, maadhimisho yatafanyika ngazi za mikoa na halmashauri kwa kutoa elimu na hamasa juu ya magonjwa haya katika jamii." Amesema.
Dkt. Clara Mwansasu ni Afisa kutoka Mpango huo wa kutokomeza magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele ameeleza kuwa, Tanzania imekuwa ikitekeleza afua za kutokomeza magonjwa hayo ikiwemo kutoa elimu na kumezesha dawa (NTD’s) baada ya kuwa imefanya tathmini ya kina.
Sambamba na hilo, ametoa wito kwa wananchi kuendelea kushiriki katika utekelezaji wa afua nyinginezo ikiwamo usafi wa mazingira na mwili kwani ni moja ya visababishi vikubwa vya magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...