Viongozi wa Mkoa wa Simiyu wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa huo Mhe. Dkt. Yahaya Ismail Nawanda Mkuu wa Wilaya ya Bariadi Mhe. Simon Simalenga @official_simalengatz watumishi , Vyombo vya Usalama Mkoa na Wilaya, wananchi, watumishi wa taasisi za serikali na watu binafsi Wameadhimisha miaka 60 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar kwa kufanya Usafi katika maeneo mbalimbali ndani ya Mji wa Bariadi, wilayani Bariadi ili kuweka Mazingira katika hali ya usafi na kuendelea kujikinga na magonjwa mbalimbali.

Mhe. Nawanda ameshiriki zoezi hilo huku akimtaka Mkuu wa Wilaya ya Bariadi Mhe.Simon Simalenga kuhakikisha anapita maeneo yote hatarishi na kufanya usimamizi ili wananchi waendelee kuweka mazingira safi na mji uendelee kuwa msafi ili kujikinga na magonjwa ya mlipuko yatokanayo na mazingira kuwa machafu.

Wilaya ya Bariadi imeendelea na kampeni yake ya kuhakikisha mazingira yanakuwa safi sehemu zote hasa katika maeneo yenye msongano.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...