NA EMMANUEL MBATILO, MICHUZI TV

SHIRIKA la Viwango Tanzania (TBS) limetoa elimu kwa umma na wafanyabiashara katika Maonesho ya Ghana EXPO Tanzania 2024 yenye lengo la kujenga ufahamu wa majukumu ya taasisi hiyo kwa wageni kutoka nchini Ghana na wenyeji kuhusu utaratibu wa kuingiza bidhaa kutoka nje ya nchi.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Januari 28,2024 Afisa Masoko wa (TBS) Bi.Rhoda Mayugu amesema kuwa wametoa elimu kwa wageni kutoka nchi ya Ghana ambao wengi waliuliza kuhusu taratibu za uingizaji wa bidhaa nchini ili kukidhi matakwa ya viwango vya Tanzania.

"Elimu hiyo imetolewa na wengi wameishukuru TBS kwani hata walipoleta bidhaa zao kwa ajili ya maonesho walipata huduma nzuri pasipo usumbufu wowote". Amesema Bi. Rhoda

Aidha Bi. Rhoda amesema wenyeji waliohufika katika banda walielezwa kuhusu taratibu za kupata alama ya ubora ambayo itawasaidia kutanua wigo wa kukuza bidhaa zao katika Ukanda wa Afrika Mashariki.

Pamoja na hayo amesema wametoa elimu kwa watembeleaji waliotaka kujifunza kuhusu maelezo ya msingi yanayopatikana katika bidhaa ambazo zinakidhi Viwango kwa ajili ya matumizi ambapo ameainisha bidhaa kuwa bora inatakiwa iwe na alama ya ubora pamoja na kuonesha muda wa matumizi wa bidhaa hiyo.

Aidha Ametoa wito kwa wazalishaji na waagizaji wa bidhaa nchini kuzalisha bidhaa zinazokidhi matakwa ya viwango na salama kwa matumizi ya binadamu.

Vilevile amewaasa watumiaji wa bidhaa nchini kusoma maelezo yanayopatika katika vifungashio vya bidhaa ili kutambua muda wa matumizi na alama ya ubora wa bidhaa, ili kuwa na uhakika bidhaa wanazonunua kama zinafaa kwa matumizi.

Kwa Upande wake Afisa Ukaguzi (TBS), Bw. Adamu Mitumba amesema kuwa bidhaa za vyakula na vipodozi vinavyotoka nje ya nchi kabla ya kuingizwa nchini muagizaji anapaswa kupeleka sampuli ya bidhaa hiyo kupimwa na shirika hilo ili zipate kibali cha kuuzwa nchini.

"Bidhaa za vipodozi na vyakula zinahitaji ziwe na usajiri kutoka TBS, kama mfanyabiasha anasafirisha bidhaa hizo kutoka nje anatakiwa kuwasilisha sampuli ya bidhaa hizo ili kupimwa na TBS na kama zinakidhi Viwango ndipo ataruhusiwan kuleta hiyo shehena na kwa bidhaa ambazo si za chakula wanatakiwa kutumia mawakala wetu katika Kanda husika". Amesema Bw. Mitumba.








Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...