Na Mwandishi Wetu 

MWENYEKITI wa Umoja wa Jamii ya Watanzania Waliostaafu Kazi ( UJAWATA), Sadiki Msuya amemuomba Rais Dk Samia Suluhu Hassan kuwaongezea pensheni ya kima cha chini kutoka Shilingi 100,000 hadi Shilingi 500,000 kwa sababu kwa sasa kutokana na hali ya maisha kupanda kiwango hicho hakikidhi mahitaji yao. 

Hayo yamesemwa leo na Mwenyekiti wa Ujawata, Sadiki Msuya wakati akizungumza na waandishi wa habari jiji Dar es Salaam, baada ya kukutana na kuzungumza na baadhi ya waastafu wa umoja huo kutokana na hali ngumu ya maisha wanayopitia. 

Pia, Msuya ameiomba serikali iushauri Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSF) kuwaongezea pensheni yao ikiwezekana ibadilishe baadhi ya vifungu vya sheria vilivyopitwa na wakati. 

"Hawa ni wastaafu waliyofanya kazi serikalini, dhumuni letu kubwa na kilio chetu ni pensheni tunaliyolipwa na mfuko wa PSSF sisi wa kima cha chini cha Sh 100,000 kwa hali halisi ya maisha ya leo ni kiwango kidogo sana hakikidhi maisha,"

"Tunaiomba Rais Dk Samia Suluhu Hassan atupe hata Sh 500,000 tunajua serikali ina mambo mengi na ina kazi nyingi za kufanya, lakini ituangalie kwa sababu na sisi tulitumikia nchi hii tukaijenga ikafika hapa Ilipofika tukapumzika tukawaachia kijiti wengine, "amesema Msuya

Amesema kuwa suala hilo wamelifutilia kwa muda mrefu bila mafanikio ndiyo maana wa kaamua kutumia vyombo vya habari kufikisha kilio chao kwa Rais kwa sababu wanajua, hajui kama kuna wastaafu wanalipwa kiwango hicho.

Kwa upande wake, Katibu wa Ujawata, Profesa Haizer Laizer aliomba mamlaka husika kuweza kuliangalia suala hilo kwa jicho la tatu ni namna gani ya kuboresha maisha ya wastaafu hawa wasiende kufa taratibu ili na wao waishi maisha stahiki yenye staha wakiwa wanauwezo wa kupata ugali wao na matibabu. 

"Kama suala ni sheria basi vifungu vya sheria za PSSF vibadilishwe kwa sababu vimepitwa na wakati kwa sababu kila siku maisha yana badilika. Tunaomba Rais asikie kilio chetu kwa kuwaongezea pensheni yetu," amesema Profesa Laizer 

Mmoja wa waastafu hao, Grace Msangi amesema wana hali mbaya ya kimaisha kwenye suala la afya, wengi wanatumia dawa kali kutokana na magonjwa yanawasumbua, lakini lishe kwao imekuwa ngumu wanashindia chai na maandazi mawili.

" Mama tunaomba usikie kilio chetu wewe ni malikia wetu wa nguvu huna baya na mtu, tunaomba ulione hili tatizo kwetu kwa sababu hali mbaya Wazee wanakunywa dawa kali sana, lishe hawana hali inayosabanisha magonjwa mengine yazalishwe," amesema Msangi.

Katibu wa Umoja wa Jamii ya Watanzania Waliostaafu Kazi (UJAWATA), Profesa Haizer Laizer akizungumza na waandishi wa habari jiji Dar es Salaam mara baada ya kumaliza mkutano na baadhi ya wanachama wa umoja huo kuhusiana na kuiomba Serikali kuwaongezea pensheni yao kutoka Sh 100,000 hadi Sh 500,000.
Mwenyekiti wa Umoja wa Jamii ya Watanzania Waliostaafu Kazi (UJAWATA), Sadiki Msuya akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, baada ya kumaliza mkutano na baadhi ya wanachama wa umoja kuhusu kufikisha kilio chao cha kuongezewa pensheni yao kwa Rais Dk Samia Suluhu Hassan.Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...