Na Mwandishi Wetu, Mbinga

BAADHI ya wananchi wa kijiji cha Utili,kata ya Utili wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma,wameuomba wakala wa maji na usafi wa mazingira vijijini(Ruwasa) kuwakabidhi mradi wao wa maji ili waweze kuhudumia na kufanya matengenezo ya miundombinu pindi inapoharibika.

Wametoa maombi hayo jana kwa kaimu meneja wa Ruwasa wilaya ya Mbinga Davis Charles,aliyetembelea mradi huo ulioanza kutekelezwa mwezi Mei 2022 na kukamilika mwezi Januari 2023.

Awadhi Meza alisema,licha ya kuanza kupata huduma ya maji,hata hivyo yanatolewa kwa mgao unaodumu kati ya siku 3 hadi 4 hivyo wanalazimika kwenda kwenye visima na vyanzo vyao vya asili.

“Tunaiomba serikali kupitia Ruwasa wilaya ya Mbinga,itukabidhi mradi huu ili tuweze kuhusimamia na kuendesha sisi wenyewe kwa kuwa umekamilika tangu mwaka jana,tunaamini tukiusimamia na kuuendesha sisi wenyewe huduma ya maji itaimarika tofauti na sasa ambako tunapata maji kwa mgao” alisema.

Alisema,wako tayari kutumia gharama zao ili mradi huo uweze kutoa huduma ya maji kwa masaa 24,na wanashindwa kufanya marekebisho ya miundombinu iliyoanza kuharibika kwa sababu bado uko chini ya mkandarasi.

Alisema,wanaumia kuona baadhi ya miundombinu ya mradi huo kama koki kwenye baadhi ya vituo vya kuchotea maji zimeanza kuharibika,huku mkandarasi hakishindwa kufunga koki nyingine jambo linalowapa wasiwasi mkubwa.

Marietha Hyera alisema, hawana imani kama kazi zilizopangwa kutekelezwa katika mradi huo zitakamilika kwa sababu ya ukimya wa mkandarasi kutoonekana eneo la kazi.

Ameiomba Ruwasa wilayani humo,kupeleka mtandao wa maji ya bomba kwenye mitaa ambayo haijafikiwa na huduma hiyo ili wananchi wa maeneo hayo wapate huduma ya maji na kufaidi matunda ya serikali yao ya awamu ya sita.

Marietha,ameshangazwa na baadhi ya vituo vya kuchotea maji(DPS) kujengwa kwenye maeneo yenye watu wachache badala ya kupelekwa kwenye mitaa yenye mikusanyiko ya watu wengi ambao watakuwa na uwezo wa kulipia huduma za kutumia maji kila mwezi.

Kwa upande wake kaimu meneja wa Ruwasa wilaya ya Mbinga Mhandisi David Charles alisema,mradi wa maji Utili umesanifiwa kuhudumia watu 3,626 na utekelezwa kwa gharama ya Sh.milioni 428,434,692.

Alitaja kazi zilizopangwa kutekelezwa katika mradi huo ni ujenzi wa tenki la ujazo wa lita 150,000, kujenga chanzo cha maji,uchimbaji wa mitaro na ulazaji wa bomba za kusambaza maji urefu wa kilomita 13.6 na ujenzi wa vituo 14 vya kuchotea maji.

Aidha, alisema utekelezaji wa mradi huo umefikia asilimia 98 na kazi zilizobaki ni uwekezaji wa mfumo wa kutibu maji na usimikaji wa alama kwenye njia za bomba za maji.

Alisema,hadi sasa utekelezaji wa mradi huo umekamilika kwa asilimia 100 na upo chini ya uangalizi wa mkandarasi ambao utaishi mwezi ujao na baada ya kipindi hicho utakabidhiwa kwa wananchi.

Amewataka wananchi wa kijiji hicho,kuhakikisha wanalinda miundombinu ya mradi huo ili uwe endelevu badala ya kuwa sehemu ya walalamikaji,kwani serikali ya awamu ya sita imetumia fedha nyingi kutekeleza mradi na kuboresha huduma ya maji kwenye kijiji chao..

 

Baadhi ya wakazi wa kijiji cha Utili kata ya Utili wilayani Mbinga,wakichota maji katika moja ya vituo(DPS)baada ya wakala wa maji na usafi wa mazingira vijijini(Ruwasa)kukamilisha ujenzi wa mradi huo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...