*Lengo kutambua michango iliyofanya Tanzania kuwa nchi ya Amani

Na Chalila Kibuda,Michuzi TV

Taasisi ya Utulivu Space inatarajia kufanya tamasha kukutanisha watu waliotoa mchango kwa Taifa la Tanzania na kufanikiwa kuwa na amani na utulivu.

Taasisi hiyo itaweza kuonyesha baadhi ya ujumbe kwa viongozi ambao walitoa mchango wao kwa kujitoa lakini wametangulia mbele ya haki.

Tamasha hilo hilo litambuliwa Utulivu Experience lenye ikiwa na watu wataoshiriki kujivunia utaifa wao wa kuwa watanzania kwa amani ilisababishwa na viongozi kuwa na maono ya mbali ya kuifanya tanzania kuwa na amani ya leo na kesho.

Akizungumza januari 30,2024 Rais wa Taasisi hiyo Ibrahim Rwegerera amesema wameamua kuja na tamasha hilo lengo kuwakutanisha watu mbalimbali waliochangia kuwapo wa amani na utulivu uliopo nchini na kuweka historia isiyofutika katika kizazi cha sasa.

Amesema tamasha hilo ni la kwanza na aina yake kufanyika katika mazingira ya kitulivu ambapo litawakutanisha watu mbalimbali wakiwemo watu maarufu ambao wana asili ya kitanzania watakaa na kujadilina na kunywa chai pamoja.

"Tamasha hili linawahusu watu wote wenye asili ya kitanzania tunawakaribisha wote wacheza mpira,wasanii,wanasiasa na kila mwenye asili ya kitanzania maana hii itakua ni siku yetu ya kusheherekea Utanzania wetu hivyo tujitokeze kwa wingi hii itakua tamasha la kihistoria"Amesema

Amesema Tamasha hilo litafanyika kwa awamu mbili ambapo awamu ya kwanza linatarajiwa kufanyika mwezi Aprili 20,2024 katika ukumbi wa Super dom Masaki na awamu ya pili litafanyika Zanzibar mwishoni mwa mwezi novemba 2024.

Kwa upande wake mmoja wa waandaaji wa tamasha hilo Mchereshaji 'MC' Anthony Luvanda amesema tamasha hilo linatoa fursa kwa wageni kuja kujifunza asili ya mtanzania ikiwemo ukarimu na utamaduni wa Mtanzania.

"Nitoe wito kwa watu wa mataifa yote kuja kujifunza asili yetu lugha yetu,mavazi yetu ukalimu na utulivu wetu waje wajifunze utamaduni wa kiswahili"amesema Luvanda.

Aidha Luvanda amesema kuwa utulivu unaanzia kwa mtu binafsi lakini unachochewa na amani iliyopo katika nchi.

Tamasha la Utulivu Experience litafanyika Aprili 20,jijini Dar es salaam katika ukumbi wa Super dom Masaki na litapambwa na wasanii wakiwemo wazamani na watu waliochangia Amani na utulivu uliopo nchini.
 

Rais wa Taasisi ya Utulivu Experience, Ibrahim Rwegerera akizungumza na waandishi wa habari  kuhusiana na tamasha la kutambua mchango wa viongozi waliofanya Tanzania kuwa na Amani na Utulivu kwenye Hoteli ya Hayatt Regecy The Kilimanjaro Hotel, jijini Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...