Umoja wa Wanawake (UWT) Ofisi ya Zanzibar umempongeza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapunduzi Mhe.Dkt. Hussein Ali Mwinyi kwa kuongeza idadi ya Wanawake katika safu ya Uongozi.

Pongezi hizo zimetolewa na Naibu Katibu Mkuu wa Umoja huo Tunu Juma Kondo katika kikao cha pamoja,kilichowashirikishi Viongozi wa UWT Zanzibar na kufanyika Ofisi kuu ya CCM Kisiwanduwi Wilaya ya Mjini.

Amesema uamuzi alioufanya Dkt. Hussein Ali Mwinyi wa kuwateuwa manaibu Mawaziri Wanawake ni wa kupongezwa kwani unaenda sambamba na matakwa Uwt katika kuhaikisha wanafikia 50 kwa 50 katika ngazi za Uongozi.

Aidha amewataka Viongozi Wanawake walioteuliwa kushika nafasi hizo kuwa wabunifu na kufanya kazi kwa bidii ili kuweza kumsaidia Mhe. Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Barazala la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwenyi katika kuleta Maendeleo.

Vile vile amewataka Viongozi hao kufanya kazi kwa nguvu zote na kushirikiana kwa hali na mali na Viongozi wengine ili kuzidi kujenga Upendo, ari na mshikamano katika Utendaji.

Naibu Katibu Mkuu huyo amewataka kuhakikisha wanahamasisha Wanawake wenzao kujitokeza kwa wingi kupiga kura katika Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika 2025 kwani idadi kubwa ya wapiga kura ni Wanawake.

Mbali na hayo amewataka Wanawake wenzake kujiendeleza zaidi kielimi ili iwe rahisi kuchaguliwa na kufikia 50 kwa 50 katika ngazi za maamuzi na kupata Viongozi wengi Wanawake watakaoweza kutetea haki zao.

Nae Katibu wa UWT Mkoa wa Kaskazini Unguja Zuwena Suleiman Mohamed na Mwenyekiti wa Umoja huo Mkoa wa Kusini Pemba Zuwena Abdallah Haji wamesema juhudi zinazochukuliwa na Dkt. Mwinyi ni kubwa kwani zinawagusa moja kwa moja Wanawake ikiwemo uimarishaji wa Sekta ya Maji, Barabara,Uchumi wa Buluu na huduma za Afya.


Hata hivyo wamesema wataendelea kuwa imara na kujipanga kuhamasisha Wanawake kujiunga kwa wingi katika Umoja huo ili kuweza kupata fursa mbalimbali zinazojitokeza ikiwemo kuteuliwa kushika nafasi za Uongozi.


Itakumbukwa kuwa hivi karibuni Rais wa Zanzibar na Mwnyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi amefanya mabadiliko ya Baraza la Mapinduzi ambapo katika mabadiliko hayo alimteua Mhe. Zawadi Amour Nassor kuwa Naibu Waziri katika Wizara ya Maji, Nishati na Madini pamoja na Mhe.Salha Mohamed Mwinjuma kuwa Naibu Waziri wa Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makaazi.


Naibu Katibu Mkuu wa UWT Ofisi Zanzibar Tunu Juma Kondo akitoa pongezi kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Hussein Ali Mwinyi kufuatia uteuzi alioufanya january 27 mwaka huu, ulioongeza idadi ya Wanawake katika nafasi za Uongozi ,hafla ilyofanyika afisi kuu ya CCM Kisiwandui Mjini Unguja.


Katibu wa UWT Mkoa wa Kusini Unguja Zuwena Suleiman Mohamed akichangia wakati wa hafla ya kumpongeza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Hussein Ali Mwinyi kwa kuongeza idadi ya wanawake katika safu ya Uongozi katika Uteuzi alioufanya January 27 mwaka huu,huko Ofisi kuu ya CCM Kisiwandui Mjini Unguja.


PICHA NA FAUZIA MUSSA –MAELEZO ZANZIBAR

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...