Na Khadija Seif, Michuziblog

TAKRIBANI Nchi saba za Afrika za hudhuria Mafunzo ya Usalama Barabarani yaliyoandaliwa na Shirikisho la Kimataifa Usalama Barabarani (ACTA) kwa siku 3 yenye lengo la kupunguza ajali na vifo vya barabarani hususani kwa Watoto mashuleni.

Akizungumza na Wanahabari Leo January 31, 2024 Mwenyekiti wa Shirikisho la Vilabu vya Usalama wa Barabarani Kimataifa kutoka nchini Botswana Simon Mang amesema dhumuni la mafunzo haya ni kuzipa uwezo klabu hizo na uelewa namna ya kufanya utetezi na kushirikiana na serikali katika kushughulikia masuala ya usalama barabarani Afrika.

Amezitaja nchi ambazo zimeshiriki Semina hiyo ambazo ni Kenya, Botswana, Namibia, Msumbiji, Nigeria, Afrika Kusini, Uganda pamoja na huku nchi mwenyeji akiwa Tanzania.

Aidha Mang ameongeza kuwa alikuwa miongoni mwa Wajumbe walioshiriki Mkutano wa Maandalizi kuomba ruzuku kutoka Taasisi ya FI ulipozinduliwa na Sir Robinson uliofanyika nchini Tanzania.

"Nilikua sehemu ya maandalizi na nilikuwa sehemu ya mshiriki na Mjumbe kwenye mkutano huo ambapo tulijadili kuomba ruzuku kutoka Taasisi ya (FI ) Kuomba ruzuku kwa ajili ya Kufanya Kampeni ya Helmenti na kufanya mafunzo ya udereva wa usalama kwa madereva wa mabasi."

Aidha amesema Vilabu vyote vilivyoshiriki katika Mafunzo hayo vitaenda kuwa mabalozi wazuri kwa nchi zao na Kuhakikisha bajeti itakayowekwa itaenda kuweka mikakati kwa namna watakavyoweza Kusaidiana na Serikali kujenga na kuboresha miundombinu barabarani.

Pia ametoa rai kwa Serikali Kuhakikisha wanaunga mkono mashirikisho hayo yanayolenga Kuhakikisha Usalama wa Barabarani kwani watu wengi wamekuwa wakipoteza maisha kwa kutokana na miundombinu mibovu iliyopo .

Kwa upande wake Muwakilishi wa Shirikisho la Usalama Barabarani Kimataifa (FIA) Aggie Krasnolucka ameeleza namna Mafunzo hayo yataleta msaada mkubwa kwa wahanga wa ajali za barabarani hasa watoto na kwa muda mfupi watatembelea klabu za usalama barabarani zilizopo mashuleni ili kusambaza elimu mbalimbali namna ya kudhibiti ajali hizo kwa kuboresha maeneo mbalimbali korofi hasa vivuko vilivyopo karibu na shule .
Mwenyekiti wa Shirikisho Usalama Barabarani Kimataifa (ACTA) Simon Mang akizungumza na Wanahabari Leo January 31,2024 wakati wa kufungua Mafunzo ya siku tatu kwa Vilabu kutoka nchi 07 za Afrika kusaidia kutoa elimu ya Usalama Barabarani


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...